• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

KAZI NZURI YA MIRADI WILAYA YA MANYONI NA ITIGI YAKONGA NYOYO ZA WAJUMBE WA KAMATI YA SIASA MKOA WA SINGIDA.

Posted on: August 20th, 2021

KAZI nzuri ya kutekeleza miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na Itigi imekonga nyoyo za wajumbe wa Kamati ya Siasa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Singida wakati walipokuwa wakikagua miradi hiyo.

Miradi hiyo imetekelezwa na halmashauri hizo kwa wakati baada ya kupatiwa fedha na Serikali ili kujenga miundombinu ya maji, ujenzi wa zahanati, miradi ya maji, madarasa na maabara.

Wajumbe hao wakizungumza kwa nyakati tofauti jana wakati wakikagua miradi hiyo walisema wamelidhishwa na utekelezaji wake licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo.

Akizungumzia miradi hiyo Mjumbe wa Kamati hiyo Diana Chilolo alisema kazi kubwa imefanyika katika kutekeleza miradi hiyo katika wilaya zote hizo mbili.

“Tumetembelea miradi mbalimbali na tumelidhishwa na utekelezaji wake na kujenga imani kwa Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ,” alisema Chilolo..

Mjumbe mwingine wa kamati hiyo Yohana Msita alisema miradi mingi iliyotekelezwa imelingana na fedha halisi walizopewa na Serikali.

“Watekelezaji wa miradi hii wameonesha uaminifu mkubwa wa matumizi ya fedha walizopewa kwa ajili ya kuitekeleza,” alisema Msita.

Martin Lissu mjumbe wa kamati hiyo alisema kasoro ndogo ndogo ambazo zimejitokeza wakati wa kujenga maabara katika baadhi ya shule za sekondari kama kuweka nondo kwenye madirisha na milango kufungukia ndani badala ya nje kwa ajili ya tahadhari ya majanga ya moto wametoa ushauri wa kuzirekebisha.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Alhaji Juma Kilimba alisema miradi hiyo inafanywa ikiwa ni utekelezaji wa ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)

 Kilimba alisema ameridhishwa na utekelezwaji wa miradi hiyo iliyofanywa katika halmashauri hizo.

“Kwa kweli tunawapongeza kwa kuitendea haki miradi hii ambayo Serikali inatumia fedha nyingi kuitekeleza,” alisema Kilimba.

Kilimba alitumia nafasi hiyo kuwaomba viongozi ilipo miradi hiyo kuwahamasisha wananchi wao kwa ajili ya kusaidia shughuli mbalimbali za kijamii badala ya kuisubiri Serikali.

Alisema Serikali inafanya kazi kubwa ya kutoa fedha za miradi na ni wajibu wa wananchi nao kuhamasika kuunga jitihada za serikali kwa kujitolea kufanya kazi zingine za maendeleo ambazo zipo ndani ya uwezo wao.

Aidha Kilimba akizungumza kwa nyakati tofauti aliwataka wananchi na viongozi waliofika kushuhudia ukaguzi huo kuendelea kuchukua tahadhari za kujikinga na ugonjwa wa corona.

Aliwaomba wananchi kila ilipotekelezwa miradi hiyo kuitunza ili iendelee kuwa na manufaa kwao.

 Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge (kulia) akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Siasa mkoa wa Singida

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.Binilith Mahenge aliomba miradi ambayo bado haijakamilika ikamilike haraka ili wananchi waanze kunufaika nayo kwani imetumia fedha nyingi kutoka Serikalini.

Miradi iliyokaguliwa na kamati hiyo katika Wilaya ya Manyoni ni ujenzi wa madarasa mawili Shule ya Msingi Heka, ujenzi wa mradi wa maji Kintinku Lusilile, ukamilishaji wa maabara Shule ya Sekondari Mlewa, kutembelea mradi wa Kilimo cha umwagiliaji Kata ya Chikuyu na kuona changamoto ya mfumo wa maji kuacha njia badala ya kwenda kwenye mashamba yana elekea maeneo mengine kutokana na mafuriko na ujenzi wa Kituo cha Afya Chibumagwa.

Katika Wilaya ya Itigi miradi iliyotekelezwa ni ukamilishaji wa maabara na vyoo Shule ya Sekondari Itigi, ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa Shule ya Msingi Mlowa na ujenzi wa mradi wa maji wa Kijiji cha Kitopeni. 

 Ziara hiyo ya ukaguzi wa miradi hiyo iliwahusisha viongozi na wataalamu mbalimbali wa wilaya hizo. 

Leo kamati hiyo itahitimisha ziara yake kwa kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

MATUKIO MBALIMBALI KATIKA PICHA

Leo tarehe 20/08/2021 kamati hiyo itahitimisha ziara yake kwa kukagua miradi ya maendeleo katika Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.