• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

KLINIKI YA SHERIA KUKATA KIU YA MASHAURI YA WANANCHI MKOANI SINGIDA.

Posted on: May 16th, 2025

Wanasheria wabobezi zaidi ya 40 kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Wizara ya Katiba na Sheria na wa Mkoa wa Singida wataweka kambi ya siku tano katika kliniki ya sheria bila malipo kwa lengo la kutoa ushauri wa kisheria kwa wananchi, watumishi wa umma na viongozi mkoani hapa.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe.Halima Dendego, amezungumza hayo leo Mei 16,2025 na waandishi wa habari wakati  akitambulisha uzinduzi wa Kamati ya Ushauri wa Kisheria ngazi ya Mkoa ambayo itafuatiwa na uendeshaji wa kliniki ya sheria bila malipo kwa wananchi wote wa Mkoa wa Singida kuanzia Mei 19 hadi 23 mwaka huu.

"Namshukuru Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kulinda, kukuza na kutetea haki za wananchi wanyonge na kupinga vitendo vya uvunjifu wa haki za kibinadamu,misingi ya utawala wa sheria, ukatili wa kijinsia na kuheshimu utawala wa sheria ambao ndio msingi wa maendeleo," amesema Mhe.Dendego.

Mhe.Dendego amesema Kamati za Ushauri wa Kisheria za Mikoa na Wilaya zimeanzishwa kwa mujibu wa sheria ya utekelezaji wa majukumu ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali sura ya 268 na mwongozo wa huduma za ushauri wa Kisheria katika ngazi ya Mkoa na Wilaya.

Amesema faida za kamati hizo za mikoa na wilaya ni kupunguza mashauri au migogoro dhidi ya serikali,huduma za ushauri wa kisheria ambazo zitakutanisha mawakili wa sheria wa taasisi mbalimbali na kuwasaidia wananchi wenye changamoto mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa amesema kuwa  faida nyingine ni uwepo wa huduma ambao utawawezesha mawakili wa serikali kusimamia utawala wa sheria katika maeneo yao,kupunguza malalamiko ya kisheria kutoka kwa wananchi, kutoa elimu ya sheria kwa umma katika kushughulikia changamoto mbalimbali na kupunguza vitendo vya uonevu na vinavyovunja sheria na taratibu.

"Nitoe rai kwa wananchi wote kujitokeza kwa wingi siku ya uzinduzi pamoja na kuhudhuria kliniki ya kisheria kuanzia Mei 19 hadi 23 na wakati wote wa kliniki kutakuwa na Kamati ya Ushauri wa Kisheria ngazi ya mkoa,Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Mawakili wa Serikali kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali," amesema Mhe.Dendego.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Sheria Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Matrider Meckson, amesema siku ya uzinduzi kutakuwa na wanasheria wabobezi kutoka ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali,Wizara ya Katiba na Sheria na wa kutoka Mkoa wa Singida.

"Tumelenga kupunguza mashauri  kwasababu kuna malalamiko mengi na pia tunataka kuhakikisha tunapunguza mashauri yanayoenda mahakamani  pamoja na wananchi kuhakikisha wanapata haki zao," amesema.

Meckson alisema wanasheria hao wabobezi ambao watakuwa zaidi ya 41 watahakikisha shauri au malalamiko ya wananchi yanafuatiliwa hadi mwisho na ufumbuzi kupatikan hivyo wenye malalamiko mbalimbali ikiwemo ya ardhi,mirathi nakadhalika.


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • "SINGIDA IMEJIPANGA KUONGOZA UFAULU KITAIFA":RC DENDEGO

    June 04, 2025
  • MRADI WA TACTIC KULETA NEEMA MANISPAA YA SINGIDA.

    June 02, 2025
  • "WAHITIMU MSIBWETEKE,JIENDELEZENI KATIKA FANI ILI MJIAJIRI"-DKT.MGANGA

    May 30, 2025
  • DKT.MGANGA:"WATUMISHI MSIKUBALI KUTUMIKA VIBAYA,KUWENI NA UTAMBULISHO MZURI"

    May 27, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.