• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Maadhimisho ya 58 ya Muungano Singida Yatumika Kuwafunda Vijana

Posted on: April 26th, 2022

Vijana mkoani Singida wametakiwa kujiamini, kuonesha na kuvitumia vipaji walivyonavyo katika kuleta ubunifu na ugunduzi wa mambo kwa kuwa wengi wana vipaji  lakini hawajavitambua.

Akiongea katika Kongamano la maadhimisho ya 58 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa Chuo cha uhasibu (NlT) uliyopo mkoani hapo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Gerry Muro amewataka vijana kuhakikisha wanatumia akili zaidi kuliko elimu katika kutambua vipaji walivyonavyo na kuchukua hatua.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Gerry Muro akizungumza na vijana wakati wa Kongamano 

Akieleza umuhimu wa vijana kutumia akili zaidi kuliko elimu DC Muro amesema kwamba duniani wagunduzi wakubwa hawakutumia elimu lakini walitumia akili na wakafika mbali hivyo kuwataka wajitume na waweze kutumia vipaji vyao kama njia ya kupitisha elimu wanazopata.

Aidha DC Muro amebainisha kwamba kijana anayemaliza chuo na kukaa mtaani akisubiri Serikali itoe ajira ni matokeo mabaya ya matumizi ya vipaji kwa kuwa kila mmoja amepewa kipaji chake.

Amewataka vijana kujiunga katika vikundi na kuvisajili ili waweze kupata mikopo kupitia asilimia Nne katika Halmashauri zao huku akiwakumbusha Maafisa Maendeleo ya Jamii kuendelea kutoa msaada wa mawazo kwa vijana wenye vikundi.

DC Muro ameendelea kusema kwamba huenda matumizi mabaya ya simu janja ndio chanzo cha vijana kushindwa kufikiria vizuri namna ya kutatua changamoto zinazowakabili ikiwemo ugunduzi wa vipaji vyao na namna ya kupata mitaji na utajiri kwa ujumla.

Amewataka vijana kutumia Kongamano kuzitumia fursa ambazo zimekuwa zikioneshwa katika mada mbalimbali zilizowasilishwa, na kila mwenye kipaji kuanza kuzitumia.

Kwa upande wake Afisa Vijana Mkoa wa Singida na mratibu wa Kongamano hilo Fredrick Ndahani amesema lengo la Kongamano hilo ni kuonesha fursa za kiuchumi ambazo zimezunguka Mkoa wa Singida ili waweze kuzitumia na kujikwamua katika maisha yao ya kila siku.

Afisa Vijana Mkoa wa Singida na mratibu wa Kongamano, Fredrick Ndahani akizungumza wakati wa Kongamano

Aidha akieleza jitihada za Serikali katika Mkoa wa Singida zakuwainua vijana amesema katika kipindi cha mwaka 2021/2022 Mkoa umetoa jumla ya Tsh. Milioni 601.4 ikiwa ni mikopo iliyotolewa katika vikundi 133.

Amebainisha kwamba jumla ya ekari 23418 zimetengwa kwa ajili ya vijana ili kufanya shughuli za uwekezaji na michezo katika Wilaya ya Manyoni Ikungi Singida na Itigi.

Afisa vijana huyo wa Mkoa akawataka vijana kuacha kutumika katika matukio ya uvunjifu wa Amani na kujihusisha na mambo ambayo yatawajengea uaminifu mkubwa.

Burudani mbalimbali zikiendele

Mwisho

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.