• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Mahakimu Mkoani Singida wakumbushwa kuwatendea haki Wananchi.

Posted on: February 1st, 2023

Mahakimu na Wasimamizi wa Sheria Mkoani Singida wametakiwa kuepuka vitendo vya kupokea rushwa ambayo unaosababishwa upindishwaji wa Sheria ili kuwatendea haki wananchi huku wakihimizwa  kusaidia kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi.

Maelezo hayo yametolea leo na Jaji Mstaafu Fatuma Massengi wakati wa kilele cha wiki wa Sheria inayoadhimishwa kila tarehe 1 February Nchini, maadhimisho ambayo Mkoa wa Singida zimeadhimishwa katika viwanja vya Mahakama ya Mkoa iliyopo mjini Singida.

Jaji Massengi amesema katika vitabu vya dini vimeeleza kwamba Mahakimu watakuwa wa mwisho kuingia mbinguni kwa kuwa maswali yatakuwa mengi hasa kwa wale ambao hawakuwatendea haki wanaanchi.

Aidha amewaasa Mahakimu kutenda haki na kusimamia Sheria kwa kuwa kazi hiyo ni kazi ya Mungu na ni msingi wa Maendeleo ya nchi ambapo kama Sheria itapindishwa itasababisha kudumaza uchumi wa nchi.

"Tuache kupokea rushwa kwa kuwa inadidimiza uchumi, napenda kuwakumbusha Mahakimu kuhakikisha wanatenda kazi ya Mungu bila upendeleo, vitabu vya dini vinaeleza kwamba Mahakimu watakuwa wa mwisho kuingia mbinguni kwa kuwa watakuwa na maswali mengi ya kujibu" Alisema Jaji Fatuma.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewaomba wanasheria wa Serikali na Binafsi kuambatana naye kila wiki ya tatu ya kila mwezi kwenda Wilayani kutatua kero za Wananchi badala ya kusubiri maofisini.

Aidha amewataka Maafisa wa Mahakama kuongeza jitihada ya kutoa elimu kwa wananchi ambao hawajui umuhimu wa kutatua migogoro yao nje ya Mahakama ili kuwapunguzia gharama kupeleka mashtaka Mahakamani ambayo yangeweza kutafutiwa kwa usuluhishi.

"Tumeanzisha utaratibu wa kuwafuata wananchi walipo kwenda kusikiza changamoto zinazowakabili hivyo niwaombe mawakili wa Serikali na Binafsi tuwe tunaambatana kwenda kutatua migogoro kwa njia ya usuluhishi walipo wananchi". Serukamba

Hata hivyo amepongeza Mahakama kwa kuwa mabingwa wa kutumia teknolojia ya Habari kutatua kuendesha mashtaka na kupunguza mrundikano wa kesi katika Mahakama zao.

Naye Hakimu Mkazi wa Mahakama kuu ya Singida Allu Nzowa amesema Mahakama imejipanga kuhakisha kwamba katika mwaka mpya wa Sheria watahakikisha haki za watu zinapatikana kwa wakati.

Nzowa amewataka wananchi kuepuka migogoro kwa sababu imekuwa chanzo cha kudidimiza uchumi kwa wananchi na kuleta umaskini kwakuwa watu wanashindwa kuendelea kuzalisha au kufanya biashara kwa sababu ya migogoro.

Awali Mkuu wa Mashtaka Mkoa wa Singida  Juma Hasani Salige alieleza kwamba wananchi wanapata changamoto kuendesha migogoro kwa gharama kubwa huku ikisababisha kupungua na kudhoofika kwa uchumi wao, huku mwakilishi wa Chama cha Mawakili wa kujitegemea (LLS) Salma Musa,  aliomba wanasheria binafsi washirikishwe kwenye utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi na kupatiwa jengo la ofisi Mkoani hapa.

Mwisho

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.