• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Makinda awasihi watanzania kutoa ushirikiano wakati wa sensa

Posted on: September 8th, 2021

Watanzania wametakiwa kutoa ushirikiano wakati wa utekelezaji wa  zoezi la Sensa ya  majaribio kwa mwaka 2021 ya watu na makazi litakalofanyika katika vijiji 13 vya Tanzania bara  katika mikoa ya Kigoma, Singida, Arusha, Dar es salaam, Mwanza, Morogoro, Mtwara, Njombe na Dodoma.

Akizungumza  na wananchi hivi karibuni katika kitongoji cha kijaroda wilaya ya Mkalama mkoani Singida Kamisaa wa Sensa ambaye pia ni spika  mstaafu wa  Bunge  la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Anna Semamba Makinda  amesema sense hiyo ya majaribio itaanza tarehe 08 mpaka 19 mwezi huu hivyo  ushiriki wa wananchi ni muhimu katika  kufanikisha zoezi hilo.

Aidha amesema zoezi la sensa ya majaribio kwa mwaka 2021 litatoa mwelekeo, fursa na changamoto katika  kujipanga na sensa ya mwaka 2022.

“Tukifanya vizuri mwaka huu  itakuwa ni dalili ya kufanya vizuri Zaidi mwaka kesho kwa sababu tutakuwa tumejifunza kutokana na  changamoto za kipindi hiki” alisema Makinda.

Amesema sense ya mwaka huu itakuwa ni tofauti na vipindi vingine ambayo ilikuwa inaishia katika ngazi ya wilaya na mkoa lakini kwa mwaka huu na mwaka kesho itakuwainafanyika hadi ngazi ya kitongoji.

Lengo la sensa hii ni kutaka kufahamu juu ya makazi majengo, anuani, idadi ya watoto, vijana na wazee ambao wapo ili waweze kuendana na bajeti ya Serikali. Alibainisha mama Makinda.

Aidha mama Makinda amesema sensa ni muhimu kwa taifa kwa sababu itasaidia kusukuma gurudumu la maendeo ya jamii, kusaidia kuratibu uwepo wa miundombinu ya shule, hospitali, barabara, makazi na hata mikopo kwa wanafunzi.

Akimalizia hotuba yake Kamisaa wa sensa Mama Makinda amewatoa hofu wananchi kwamba makarani watakaohusika katika zoezi hilo wamepata mafunzo ya kutosha na wamekula kiapo cha kutunza siri za  watu wakati wa kuhesabu.

Naye mratibu wa sensa katika ngazi ya mkoa wa Singida Bw. Naeng’oya Kipuyo amesema maandalizi ya  sense  mkoani hapo yamekamilika kwa kuwa tayari maeneo yameshatengwa na uhamasishaji umefanyika kwa kiasi kikubwa.

Amebainisha kwamba sensa ya majariibio kwa mkoa wa Singida itafanyika kwa muda wa siku tatu kuanzia tarehe nane (8)   mpaka  10 ambapo wataalamu watangazia huduma za kijamii zinazopatikana  eneo hilo.

Usiku wa tarehe 10 kumkia tarehe 11 itafanyika sense ya majaribio katika Kitogoji hicho kuhesabu watu waliolala katika nyumba zao zoezi litakalochukua siku tatu (3) mpaka tarehe 13 alibainisha bwana Kipuyo.

Amesema tarehe 14 mpaka 16 zoezi la sensa litaendelea katika Kitogoji hichio cha Kijaroda ambapo itafanyika sense ya majengo, wamiliki na huduma zinazofanyika katika nyumba hizo na mwisho ilatakuwa  ni kuchukua anuani za makazi kwenye kila nyumba alimalizia bwana Kipuyo.

Mery christiani ni msichana mkazi wa Kitogoji hicho ameishukuru Serikali kwa hatua hiyo na kuwasihi wananchi kutokuwa waoga na kuhakikisha wanajitokeza kuhesabiwa ikiwa ni  pamoja na wenye mahitaji maalumu ili waweze kupata  mahitaji yao ya baadae .

Mwisho

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • "SINGIDA IMEJIPANGA KUONGOZA UFAULU KITAIFA":RC DENDEGO

    June 04, 2025
  • MRADI WA TACTIC KULETA NEEMA MANISPAA YA SINGIDA.

    June 02, 2025
  • "WAHITIMU MSIBWETEKE,JIENDELEZENI KATIKA FANI ILI MJIAJIRI"-DKT.MGANGA

    May 30, 2025
  • DKT.MGANGA:"WATUMISHI MSIKUBALI KUTUMIKA VIBAYA,KUWENI NA UTAMBULISHO MZURI"

    May 27, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.