• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

MANYONI NA ITIGI KUNUFAIKA NA UTUNZAJI WA MISITU YA ASILI.

Posted on: December 9th, 2024

Wilaya za Manyoni na Ikungi katika Mkoa wa Singida zinatarajiwa kupokea mabilioni ya fedha kutokana na utunzaji wa misitu ya asili vikiwamo vichaka vya Itigi (Itigi Thickets) ambavyo ni adimu duniani na katika Bara la Afrika vinapatika Tanzania na Zambia pekee.

Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mheshimiwa Halima Dendego, amesema hayo  wakati wa maadhimisho ya miaka 63 ya Uhuru wa Tanzania Bara ambayo yaliadhimishwa kwa viongozi wa chama, serikali na wananchi kupanda miti 501 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida.

Kabla ya zoezi la kupanda miti katika hospitali hiyo kufanyika, Dendego aliongoza viongozi wa chama, serikali na wananchi kutembelea katika wote za wagonjwa kuwapa faraja na kuwapa zawadi mbalimbali.

Mhe.Dendego Amesema mkakati mwingine uliopo ni kutengeneza mpango wa matumizi ya ardhi, kuendelea kuhifadhi misitu ya asili kwani misitu ni fedha kutokana na biashara ya hewa ukaa yenye faida nyingi na Mkoa wa Singida utakuwa miongoni mwa wanufaika wa fedha hizo.

“Wilaya yetu ya Manyoni na Ikungi ipo mbioni itaanza kupokea mabilioni ya fedha muda mchache ujao, niwapongeze wakuu wa wilaya kwa kupambana maana wananchi wetu wakiona kitu ndo wataamini, miti yetu ni dhahabu ya kijani,” alisema.

Dendego alisema mkoa utaendelea na zoezi la kuhamasisha upandaji miti zoezi rasmi la upandaji litafamnyika Januari  2025 na kuhamasisha matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kunusuru misitu.

“Vipo vijimisitu vya asili au vichaka vya Itigi, Manyoni  na Ikungi, tunaviona kama ni maeneo hatarishi lakibi kumbe ni mazalia ya tembo,yaani  tembo anapotaka kuzaa ndo anakwenda kwenye vile vichaka,” alisema.

Awali Afisa Maliasili Mkoa wa Singida, Charles Kidua alisema miti 13,399,031 ambayo ni kati 33,253,602 iliyopandwa katika Mkoa wa Singida katika kipindi cha kuanzia 2019 hadi 2024 imekufa kutokana na sababu mbalimbali ikiwamo utunzaji hafifu.

“Katika uhifadhi wa misitu na mazingira mkoa umepanda jumla ya miche ya miti 33,253.602 sawa na asilimia 63 ya lengo kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita na miti iliyopona ni 19,854,571 sawa na asilimia 59.7 ya miti iliyopandwa,” alisema.


Kidua alisema sababu za miti mingi inayopandwa kufa ni kutokana na uharibifu unaofanywa na mifugo, utunzaji hafifu,mchwa kuharibu miche, kuwepo kwa vipindi virefu vya jua na uelewa mdogo wa wananchi juu ya matumizi ya nishati safi ya kupikia.

Alisema katika kipindi hiki cha mvua miti 1,768,192 imepandwa katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Singida ambapo mkoa utaendelea na zoezi la upandaji miti ipatayo 5,395,909 katika vyanzo vya maji,taasisi za serikali,watu binafsi na taasisi za kidini hadi mwisho wa msimu huu wa mvua.

Kidua alisema katika kuhifadhi mazingira mkoa umejiwekea dira na mwelekeo kwa kuongeza utekelezaji wa upandaji miti kutoka asilimia 63 ya sasa mpaka asilimi 90 ifikapo 2030 na kuongeza idadi ya misitu ya hifadhi kufikia hekta 100,000 ifikapo 2030.


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.