• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

MAONESHO YA SABA YA MIFUKO NA PROGRAMU ZA UWEZESHAJI YAMEFUNGULIWA RASMI MKOANI SINGIDA

Posted on: September 10th, 2024

Maonesho ya Saba ya Mifuko na Programu za Uwezeshaji yamefunguliwa rasmi mkoani Singida na Waziri wa nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Mhe. William Lukuvi, ambapo katika hotuba yake amesisitiza umuhimu wa elimu ya kujitegemea huku akiwahimiza wananchi kujitokeza kujifunza kupitia maonesho hayo ili kujikwamua kiuchumi.

Akizungumza (Septemba 10, 2024) kwenye hafla ya ufunguzi wa maonesho hayo Waziri Lukuvi amewasihi wananchi wa Singida na maeneo ya jirani kutumia fursa hii kujifunza na kuimarisha biashara zao kwa lengo la kujipatia kipato na kuboresha maisha yao.

“Serikali imewaletea elimu ya kujitegemea, jitokezeni kujifunza kupitia maonesho haya ili kujikwamua kiuchumi. Mfanyabiashara mdogo jifunze kuwa mkubwa…., nawasihi muulize maswali na msubutu,” amesema Waziri Lukuvi.

Asisitiza kuwa, maonesho hayo ni fursa adhimu kwa wananchi, wajasiriamali, na vikundi mbalimbali kujifunza kuhusu fursa za uwezeshaji, kupata elimu ya kifedha, na kujionea bidhaa na huduma mbalimbali kutoka mifuko na taasisi zinazowezesha wananchi ambapo kutakuwa na bidhaa za wajasiriamali, semina za ujasiriamali uboreshaji wa biashara na ushauri wa moja kwa moja kutoka kwa wataalamu.

Akitoa salamu za Mkoa wa Singida, Mkuu wa Mkoa huo, Mhe. Halima Dendego amekiri kuwa mmoja wa mashuhuda wa hatua za Serikali inazochukua ili kuwawezesha wananchi kiuchumi hususan katika wa Singida.

" Hakuna asiyejua au kufaidika na elimu bila malipo, ruzuku za mbolea, viuatilifu na mbegu bora za alizeti, umeme vijijini, zahanati vijijini, vituo vya afya na mahospitali yenye vifaa tiba vya kisasa kabisha, wataalamu bobezi, na dawa muhimu, huduma za maji safi na salama, mabarabara, vivuko, madaraja yanayojengwa" Amesema RC. Dendego

Amesema pia kupitia fursa za uwezeshaji wananchi kiuchumi chini ya program ya kuzifikia kaya zisizojiweza, yaani TASAF, umewezesha kufikiwa kwa zaidi ya kaya 58,000 huku fedha zaidi ya shs. 22 bilioni zikitumika.

Amesisitiza kuwa utoaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa wanawake, vijana na watu wenye ulemavu  zimetolewa huku  shs. 2.5 bilioni kutengwa kwa ajili ya walengwa, aidha vikundi 7 vya vijana kufaidika na fedha za mfuko wa vijana chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu.

RC. Dendego amesema kwamba maonyesho haya yanakuja kuongeza kasi ya kuziangazia fursa za kiuwezeshaji na kama  mkoa wa Singida watahakikisha kuwa wanatumia fursa zilizopo za ndani na nje ili  kuendelea kukuza uchumi wa mkoa na wananchi wake huku akitoa rai kwa  wananchi wa mkoa huo kuendelea kuunga mkono juhudi za Serikali za kuwaletea maendeleo.

Naye, Katibu Mkuu wa baraza la Taifa la uwezeshaji (NEEC) Bi. Bein'g Issa amesema, kuongezeka kwa  hamasa ya wananchi kutafuta vigezo vya kukopesheka pamoja na kujiunga kwenye vikundi vya kiuchumi kama SACCOS na VICOBA itawakutanisha wajasiriamali na watoa huduma mbalimbali wa Serikali na binafsi watakaosaidia kuongeza thamani  na kukuza biashara zao.

Bi. Being amesema, wana  mategemeo ya kuwa na  shughuli za kutangaza fursa za mifuko hiyo pamoja na Taasisi nyingine wezeshi, kutoa mikopo kwa wajasiriamali, kuuza bidhaa za wajasiriamali pamoja na kutoa mafunzo ya uendelezaji biashara kwa wajasiriamali.

"Mpaka sasa Baraza linaratibu jumla ya Mifuko ya Uwezeshaji na Programu 72 ambayo 62 ipo Serikalini na 10 ipo Sekta binafsi, hivyo lengo kuu la Maonesho haya ni kutoa uelewa wa fursa za Mifuko kwa Wananchi ambapo ilionekana mifuko mingi haifahamiki kwa wananchi hivyo kuchelewesha kufikisha huduma za uwezeshaji kwa wananchi" Bi.Bein'g.

Maonesho hayo yanatarajiwa kuendelea kwa siku saba ambapo kilele ni tarehe 14 Septemba, 2024  na yanatoa nafasi kwa wananchi kujifunza kujipatia mbinu mpya za kujiendeleza kiuchumi kupitia mifuko na programu mbalimbali za uwezeshaji zinazotolewa na serikali kwa kushirikiana na wadau wengine.


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.