• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

MKUU WA MKOA WA SINGIDA DKT. REHEMA NCHIMBI AWAAPISHA WAKUU WAPYA WA WILAYA MKOANI SINGIDA

Posted on: July 31st, 2018

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Dkt. Rehema Nchimbi leo tarehe 31Julai, 2018 amewaapisha wakuu wapya wawili wa Wilaya  walioteuliwa na Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli tarehe 28 Julai, 2018.


Wakuu wa Wilaya walioapishwa leo katika viwanja vya ofisi ya mkuu wa mkoa Singida ni Bw. Pasacas Muragiri ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Singida, Bibi. Rahabu Mwangisa Solomon ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Manyoni.

Hafla ya kuapishwa kwa wakuu hao wa Wilaya imehudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Mhe. Miraji J. Mtaturu,  Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mhandisi. Jackson Masaka na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Mhe. Emmanuel Luhahula, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Viongozi mbalimbali wa Chama (CCM), Dini, Wakurugenzi wa Taasisi mbalimbali mkoa Singida, Wawekezaii pamoja na Wakuu wa Idara katika Sekretarieti ya Mkoa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi amewataka wakuu wa wilaya wateule kwenda kuchapa kazi na kutatua kero za wananchi katika wilaya zao huku wakizingatia kufanya kazi kwa uadilifu na uaminifu.

Dkt. Nchimbi pia amewataka kusimamia ukusanyaji mapato (kodi) ya Serikali na matumizi ya fedha na rasilimali nyingine za umma sambamba na kuhakikisha vitendea kazi vipo (POS Machine), pia  kuhakikisha wananchi wapo salama na pia kuhakikisha wananchi wanafanya kazi za uzalishaji mali.


"Sio vizuri kiongozi anakuja halafu wananchi wanalalamikia tunakero flani  tunakero flani  tunakero flani tunakero flani, inamaana sisi hatutoshi wakati sisi tupo, wakuu wa wilaya wapo, nami sitaki kuonekana sitoshi, NINATOSHA" Amesema Dkt. Nchimbi


Dkt. Nchimbi amewasihi wakuu wa wilaya kutosubiri migogoro iwafuate mezani bali kufuata wananchi pale kwenye migogoro kushughulikia haraka iwezekanavyo. 


"Usisubiri migogoro ikufuate mezani, wewe toka na nenda kaiangalie hiyo migogoro ndio utakapoona na kuifahamu katika uasilia wake, jitihada kubwa ya Serikali ya awamu ya tano, ni kuhakikisha migogoro inatoweka kwa wananchi, tusiruhusu migogoro itokee kwa wananchi" amesema Dkt. Nchimbi.


Aidha amewataka wakuu wa Wilaya kusimamia miradi yote inayotekelezwa mkoani Singida na kuiorodhesha miradi yote inayotekelezwa katika wilaya zao pamoja na kuifuatilia kwa kuzingatia tarehe ya kuanza mradi, thamani ya fedha ya mradi, unatarajia kuisha lini? na hatua zake mbalimbali.


"Wakuu wa Wilaya msisubiri taarifa za maandishi, zimetuchelewesha sana, tupate taarifa za makaratasi lakini kikubwa tunataka taarifa za yanayoonekana kwa macho, tusisubiri mpaka mhusika ametuharibia" alisisitiza Dkt. Nchimbi



Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.