• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

MRADI WA TACTIC KULETA NEEMA MANISPAA YA SINGIDA.

Posted on: June 2nd, 2025

Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais – TAMISEMI Mhe. Zainab Katimba (Mb)  Amewasihi wananchi wa Manispaa ya Singida kutoa ushirikiano kwa Mkandarasi anayetekeleza mradi wa TACTIC pamoja na kutunza miundombinu inayojengwa pale itakapokamilika ili iweze kuwa na tija iliyokusudiwa na kudumu  kwa muda mrefu zaidi, akiziagiza Halmashauri zote zenye miradi ya TACTIC kusimamia vyema uendeshaji wa masoko na Vituo vya Mabasi ili kuzalisha mapato yaliyotarajiwa na Serikali kwa maendeleo ya maeneo yao.

Mhe.Katimba amesema kukamilika kwa utekelezaji wa miradi ya uboreshaji miundombinu ya Miji Tanzania (TACTIC) awamu ya pili Kwenye Manispaa ya Singida kutaleta mabadiliko chanya kwenye huduma, manunuzi na mazingira bora ya kufanyia biashara kwa wajasiriamali na wafanyabiashara wa Mkoa wa Singida.

Ameyasema leo Juni 2,2025 katika hafla ya utiaji saini Miradi ya  Ujenzi wa Soko la Kimataifa la Vitunguu katika viwanja namba 835 na 836, Mtaa wa Misuna, lenye jumla ya mita za mraba 14,465. Jengo la ghorofa mbili, barabara za mzunguko zenye urefu wa mita 700 zitakazojengwa kwa kiwango cha lami,Ujenzi wa Barabara za Mjini Kati na Viwandani, zinazolenga kurahisisha usafirishaji wa bidhaa na huduma na Ujenzi wa Mtaro wa Maji ya Mvua Mnang’una unaotarajiwa kuzuia mafuriko na kulinda mazingira ya mijini.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, ametumia jukwaa hilo kueleza dhamira ya Mkoa wa Singida kujiimarisha kiuchumi na kuchangia kwa kiasi kikubwa pato la taifa. 

"Sisi ni majirani wa Makao Makuu ya nchi, Dodoma. Hivyo tumeamua kutumia nafasi yetu ya kijiografia kuwa mkoa wa mfano na kuwa jiji tarajiwa la kanda ya kati," amesema Mhe. Dendego.

Ameongeza kuwa, Mkoa wa Singida umeendelea kuwa mwenyeji mzuri wa wageni na wawekezaji, hasa baada ya kuwa mwenyeji wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Mei Mosi, ambapo watu kutoka ndani na nje ya nchi walifika na kuvutiwa na fursa zilizopo akisema kuwa ushirikiano baina ya serikali, sekta binafsi na wananchi ndio nguzo ya mafanikio hayo. 

"Sisi wana Singida tumeamua kupindua meza na kuwa mkoa bora Tanzania. Tuna kila sababu ya kufanikiwa; rasilimali tunazo, nia tunayo, na Mungu ametujalia ardhi nzuri, dhahabu, mazao ya chakula na biashara pamoja na mifugo," amesema Mhe.Dendego

Mhandisi Humphrey Kanyenye, Mratibu wa miradi ya Benki ya Dunia, TARURA amewataka Wakandarasi wazawa  kujitokeza kwa wingi kuomba tenda mbalimbali za utekelezaji wa miradi ya uboreshaji miundombinu ya Miji ya Tanzania (TACTIC) ili kuweza kunufaika na fursa hiyo kama sehemu ya kukuza uchumi wa Tanzania na kuimarisha mzunguko wa fedha nchini.

"Maeneo mengi tumepata wakandarasi wa Kichina lakini kwa Manispaa ya Singida tumepata bahati ya kupata mkandarasi mzawa na yeye pia amefanya kazi maeneo mengine na katika kulinganisha utendaji kazi wake kulinganisha na wakandarasi wa Kichina, Mkandarasi huyu yupo mbele kwa asilimia zaidi ya 20, “ amesema mhandisi Kanyenye.

Kulingana na mhandisi Kanyenye, kukamilika kwa mradi wa TACTIC kutaleta manufaa makubwa kwa Manispaa ya Singida ikiwemo kuongeza fursa za ajira, kuchochea ukuaji wa uchumi, na kuboresha hali ya biashara katika maeneo husika, hivyo kuchangia maendeleo ya muda mrefu ya jamii na Taifa kwa ujumla.

Soko la Kimataifa la Vitunguu litajengwa mkoani Singida likitarajiwa kuwa na jengo la ghorofa mbili likiwa na eneo la kuchambua vitunguu, kukaushia vitunguu, maduka 10, Vyumba 4 vya huduma za kifedha, pamoja na maeneo mengineyo likitarajiwa kuongeza mapato ya Halmashauri kutoka Milioni 300 hadi Milioni 505 litakapokamilika.

Mradi huo unaotekelezwa na Mkandarasi mzawa M/s Sihotech Engeneering Company Limited kwa kushirikiana na kampuni ya AMJ Global Mult Contractors kwa gharama ya shilingi 24, 748,966,236.05 na unatarajiwa kukamilika mara baada ya kipindi cha miezi kumi na tano kitakachoanza Juni mwaka huu.


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • "SINGIDA IMEJIPANGA KUONGOZA UFAULU KITAIFA":RC DENDEGO

    June 04, 2025
  • MRADI WA TACTIC KULETA NEEMA MANISPAA YA SINGIDA.

    June 02, 2025
  • "WAHITIMU MSIBWETEKE,JIENDELEZENI KATIKA FANI ILI MJIAJIRI"-DKT.MGANGA

    May 30, 2025
  • DKT.MGANGA:"WATUMISHI MSIKUBALI KUTUMIKA VIBAYA,KUWENI NA UTAMBULISHO MZURI"

    May 27, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.