• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MADINI AMALIZA MGOGORO WA UMILIKAJI MGODI KWA DAKIKA 120

Posted on: September 23rd, 2021

NAIBU Waziri Wizara ya Madini Profesa Shukuru Manya katika hali ambayo haikutegemewa na wengi ametumia masaa mawili sawa na dakika 120 kumaliza mgogoro wa muda mrefu wa umilikaji mgodi wa uchimbaji dhahabu katika machimbo ya Kijiji cha Matongo yaliyopo wilayani Ikungi mkoani hapa.

Mgogoro huo ambao umemalizwa na Profesa Manya ulikuwa ukimuhusisha mmiliki halali wa mgodi huo Richard Lyamuya na wabia wenzake Israel Njiku na Helena Mtaturu ambaye alikuwa mlalamikaji na mmiliki wa eneo hilo la mgodi lenye ekari 70 ambalo alidai lilichukuliwa na Lyamuya bila ya kufuata taratibu kwa kumuhusisha Mtaturu na ndugu zake.

Kutoka na madai hayo Mtaturu ambaye ni mjane alimuandikia barua Waziri Wizara ya madini akidai kuwa kwa kificho bila yeye kujua mmiliki wa mgodi huo Richard Lyamuya ambaye ni mkazi wa Singida Mji alikwenda ofisi za madini Mkoa wa Singida ili apewe kibali cha kuchimba dhahabu kwenye eneo lake bila ya kushirikishwa.

Baada ya barua hiyo kufika katika wizara hiyo na kufanyiwa uchunguzi ndipo jana Naibu Waziri Wizara ya Madini Profesa Shukuru Manya alipofika kwenye mgodi huo na kufanya mkutano wa hadhara uliowahusisha wadau wa uchimbaji, Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro, Viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi (CCM) wananchi na wamiliki wa mgodi huo ambao baadhi yao waliweza kuelezea walivyokuwa wakielewa jinsi mmiliki wa mgodi huo alivyopata eneo hilo kwa kufuata sheria za uchimbaji wa madini kwa kumshirikisha Helena Njiku na kuweka kumbukumbu za makubaliano kwa maandishi na kutiliana saini.

Mmoja wa viongozi wa Umoja wa wachimba madini katika wilaya hiyo (SIREMA) Seleman Omari alisema mbele ya Naibu Waziri Wizara ya Madini kuwa anaujua mchakato mzima wa uanzishwaji wa mgodi huo na kuwa hakukuwa na udanganyifu wowote na wabia hao waliwekeana namna ya kulipana ambapo Mtaturu aliachiwa asilimia 40 huku Richard Lyamuya na Israel Njiku wakichukua asilimia 30 kila mmoja.

Mbali ya Omari kuyasema hayo Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro alisema suala hilo alilikuta ofisini kwake baada ya kusikilizwa na mtangulizi wake Edward Mpogolo ambaye amehamishiwa Wilaya ya Same ambapo nyaraka zote zinaonesha umiliki wa mgodi huo ni wa watu hao watatu na tayari Serikali imekwisha wapa leseni ya uchimbaji na si vinginevyo.

Baada ya watu mbalimbali kutoa maelezo yao na kubaini kuwa Mtaturu aliandika barua ya madai ambayo sio ya kweli Naibu Waziri Profesa Manya alimwambia asirudie tena kufanya jambo hilo.

Profesa Manya alitumia nafasi hiyo kuwaomba wachimbaji hao kufanya kazi zao kwa upendo na kufuata sheria za uchimbaji.

Mkuu wa wilaya hiyo Jerry Muro aliwaomba wachimbaji hao kudumisha amani na kujikinga na

magonjwa ya Corona na ukimwi kutokana na mwingiliano mkubwa wa watu katika eneo hilo.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.