• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

RAIS DKT. JOHN MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA DARAJA LA MTO SIBITI LINALOUNGANISHA MKOA WA SIMIYU NA SINGIDA NA KUMTAKA MKANDALASI KUHAKIKISHA ANAMALIZA KAZI YA UJENZI WA DARAJA MAPEMA

Posted on: September 10th, 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli amemwagiza Mkandarasi wa Kampuni ya HAINAN kutoka CHINA kuhakikisha anafanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ujenzi wa daraja la mto SIBITI ambayo linaunganisha mikoa ya Singida na Simiyu ili kuondoa adha kubwa wanayopata wananchi hasa kipindi cha mvua.

Rais Magufuli ametoa agizo hilo mapema leo alipokuwa Mkoani Singida wakati anaweka jiwe la msingi katika ujenzi wa Daraja la mto Sibiti baada ya kutoridhika na maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo ambalo limechukua zaidi ya miaka sita licha ya mkandarasi kulipwa zaidi ya asilimia 90 ya gharama za ujenzi wa daraja hilo ambalo ujenzi wake unagharimu shilingi za kitanzania bilioni 16.

Rais MAGUFULI pia amewataka watendaji wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kumsimamia ipasavyo mkandarasi huyo ili aweze kukamilisha ujenzi huo kabla ya mwezi wa TATU mwakani na kama mkandarasi atashindwa kukamilisha kazi hiyo kwa muda ulipangwa basi atachukua hatua zaidi dhidi ya wahusika akiwemo mkandarasi huyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwele amesema ujenzi wa daraja la Mto Sibiti utakuwa ni mkombozi mkubwa kwa Wananchi wa mikoa ya Singida na Simiyu katika uimarishaji wa shughuli za kiuchumi kwenda ukanda huo.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Rehema Nchimbi kwaniaba ya wananchi wa Mkoa wa Singida amemshukuru Mheshimiwa Rais Dkt. John Magufuli pamoja na Serikali ya awamu ya Tano kwa kuifanyia mambo mengi ya kimaendeleo mkoani hapa."Serikali imetupatia jumla ya shilingi za kitanzania bilioni ishilini na nne katika masuala ya Elimu ya kuwezesha Elimu bure kwa Wananchi, ukarabati wa miundombinu ya shule, ujenzi wa hosteli na mikakati mingine ya Elimu Bure, hizi ni fedha nyingi na zimefanya mambo makubwa sana mkoani Singida." 

"Tumepokea pikipiki 136 kwa ajili ya waratibu wa elimu za Kata na tayari zimeshagawanywa na sehemu zingine zinaendelea kugawanywa. Pia tumepokea fedha za ujenzi wa vituo vya Afya ambavyo ni 10 pamoja na fedha za kutandaza nguzo za umeme vijijini. Hii ni Singida njema sana." Dkt. Nchimbi.

Aidha, Wananchi wa mikoa ya Singida na Simiyu wamemshukuru sana Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli kwa ujenzi wa daraja hilo  ambalo kwa kupitia Serikali ya Awamu ya Tano imeweza kutoa shilingi za kitanzania bilioni 16 ili Wananchi wake waweze kunufaika kwa miundombinu bora ya barabara ambapo kwa ujenzi huo wa daraja litasaidia kuongeza na kuimarisha uchumi. "Tunamshukuru Rais Magufuli kwa kuweka jiwe la msingi la daraja hili na hii inaonyesha jinsi gani Mheshimiwa Rais wa Awamu ya Tano, Dkt. John Magufuli anavyotekelea kwa vitendo ILANI YA CCM kwani daraja hili litakuwa mkombozi kwetu wananchi wa Singida na Simiyu pamoja na wananchi kutoka pande za Tanzania kwani hapa kuna shughuli nyingi sana za kibiashara hususani CHUMVI hupatikana kwa wingi sana na kwa bei rahisi" Wananchi Sitibi.


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.