• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

RAS Singida akemea ucheleweshaji wa malipo ya vibarua

Posted on: May 30th, 2023

Ucheleweshaji wa fedha na  malipo kidogo kwa vibarua na mafundi yanayolipwa  na wakandarasi katika  miradi ya ujenzi wa nyumba ya kuhifadhia maiti (Mochwari) pamoja na wodi ya wanawake na wodi ya wanaume zinazojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Manyoni mkoani Singida umechangia ucheleweshaji wa ukamilishwaji wa mradi huo jambo ambalo viongozi wameagiza kukomeshwa hali hiyo.

Akiongea baada ya ukaguzi wa majengo hayo na kusikiliza malalamiko ya baadhi ya vibarua na mafundi ambao walilalamikia kutolipwa fedha zao kwa wakati na kulipwa ujira mdogo, Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga leo amezitaka kamati za ujenzi kukutana na mkandarasi wa majengo hayo na kuwalipa madeni yao kwa vibarua na mafundi wanaofanya kazi hiyo pamoja na kukaa mezani na kukubaliana malipo mapya ili kuondoa migomo baridi ya vibarua hao.

Aidha RAS amesema kwamba hayupo tayari kuona fedha za Seriki zinarudi hazina mwisho wa mwaka wakati miradi ya maendeleo ya wananchi haijakamilika hivyo kumuelekeza Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo  Furaha Mwakafwila  kukutana na Mkandarasi huyo na kuona kama inawezekana kuachia jengo moja kwa mafundi wengine ili kazi ziweze kukamilika kwa wakati.

"Kila fundi anatakiwa kuwalipa vibarua wake kwa wakati na stahili walizokubaliana tofauti na hivyo itakuwa ni sababu ya ucheleweshaji wa kazi, na tulishatoa maelekezo kwamba fundi mmoja jengo moja kama inawezekana Mkandandarasi ashauriwe awaachie mafundi wengine jengo moja"

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya Furaha Mwakafwila amemuahidi Katibu Tawala huyo kwamba watakutana na Makandarasi kujadili namna ya kuboresha hali ujenzi, malipo ya vibarua na kuhakisha kazi inakamilika ndani ya wakati.

Hata hivyo RAS alitembelea Mradi wa Ujenzi wa shule ya Eka iliyoko Kata ya Eka Wilayani Manyoni chini ya Mradi wa Boost unaogharimu jumla wa Milioni 493.4 wenye vyumba vya madarasa  14 na Awali viwili na jengo la Utawala ambapo amewataka watendaji wa vijiji na kata kuhamasisha wananchi  kuchangia nguvu kazi lengo likiwa fedha zilizotolewa zinatosheleza.

Hata hivyo RAS Dkt. Fatma ametoa maagizo kwa wasimamizi wa ujenzi wa miradi ya boost Mkoani hapo kuhakikisha mafundi wanakuwa na mipango kazi katika eneo la kazi itakayoonesha namna ya utekelezaji wa shughuli za kila siku tofauti na hivyo mafundi wataonekana wanafanya kazi kila siku lakini majengo hayaendelei.

Hata hivyo RAS amesema Serikali kwa kiasi kikubwa imetambua umuhimu na mchango wa mafundi wa mtaani ndio maana imeendelea kuwapa kazi hivyo kuwataka kutopoteza imani hiyo kwa kufanya kazi nzuri, kutofanya uharibifu wa vifaa vya ujenzi na kubakiza kazi kwa wakati na kwa ubora unaotakiwa.

Awali RAS amewaeleza walimu katika miradi hiyo kuhakikisha wanapanda miti ya kivuko na matunda  maeneo yanayowazunguka ikiwa ni pamoja na kuyapendezesha maeneo kwa kutengeneza bustani za maua.


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.