• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

RC DENDEGO, SERIKALI ITALIPA MADENI YENU CHAPENI KAZI.

Posted on: May 1st, 2024

Mkuu wa mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego, amewaagiza Waaajiri wote mkoani humo kuhakikisha wanaruhusu Mabaraza ya Wafanyakazi kufanyika sehemu za kazi ili kujua changamoto na matatizo yanayowakabili wafanyakazi kwa nia ya kutafutia ufumbuzi haraka matatizo yanayowakabili nia ikiwa ni kuongeza ari na ufanisi sehemu za kazi.

Mkuu huyo wa mkoa wa Singida ametoa kauli hiyo katika Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika Kimkoa wilayani Ikungi Mei 1, 2024 katika viwanja vya standi ya zamani.

RC Dendego, amesema Mabaraza ya wafanyakazi yanafaida kubwa kwa sababu yanarahisisha kujua changamoto za Wafanyakazi zinazoweza kusababisha kuzorota kwa ufanisi wa kazi hivyo changamoto zikitafutiwa majawabu mapema zisaidia wafanyakazi kuongeza bidii na ufanisi kazini.

“Mimi sio Muumini wa Watu wanaovunja Sheria hivyo Waajiri Wakatakao kaidi Maagizo yangu nitashughulika nao” Amesisitiza RC. Halima Dendego.

Aidha, Mkuu wa mkoa wa Singida ameonya kuhusu Waajiri ambao hawaruhusu  wafanyakazi wao kuanzisha au kujiunga na Vyama vya Wafanyakazi na kusititiza kuwa jambo hilo ni kinyume cha taratibu na lazima likomeshwe haraka.

Kuhusu, Madeni ya Wafayakazi Mkoani Singida, Dendego amesema mkoa huo unaendelea na mchakato wa kulipa madeni ya wafanyakazi na kusema kuwa Wafanyakazi wa mkoa huo walikuwa wanaidai Serikali zaidi ya Shilingi Bilioni 1.9 na mpaka sasa Serikali imewalipa Wafanyakazi zaidi ya shilingi Milioni 700.

Amesema dhamira ya Serikali ya kulipa madeni ipo pale pale kinachotakiwa ni uvumilifu tu.

Halima Dendego amewataka Waajiri wahakikishe wanaacha tabia ya kuzalisha madeni mapya ikiwemo kuhamisha watumishi bila stahiki zao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama Vya Wafanyakazi  Tanzania ( TUCTA) mkoa wa Singida Bi. Agnes Lucas ameishukuru Serikali kwa kuendelea kulipa madeni ya Wafanyakazi, upandishaji wa madaraja na kuboresha mazingira ya kufanyia kazi ikiwemo kuwapatia vitendea kazi vya kisasa hali ambayo imesaidia kuongeza ari na uwajibikaji Sehemu za kazi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego (kulia) akiteta jambo na Katibu Tawala Mkoa huo Dkt. Fatuma Mganga kwenye hafla ya kusherehekea Maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani yaliyofanyika kimkoa Wilayani Ikungi


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.