• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

RC Mahenge Agawa Pikipiki 166 kwa Maafisa Kilimo Mkoani Singida.

Posted on: June 13th, 2022

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge leo amekabidhi pikipiki 166 kwa Maafisa Ugani wa Halmashauri za Mkoa huo kama sehemu ya vitendea kazi na kuwataka kufanya mabadiliko makubwa kwenye sekta ya kilimo na ufugaji huku akisisitiza upatikanaji wa takwimu sahihi kwakuwa itakuwa rahisi  kuwafikia wakulima walipo.

Akizungumza kabla ya kukabidhi pikipiki hizo Dkt. Mahenge amesema pikipiki 161 zitakabidhiwa kwa Maafisa Ugani wa Halmashauri za Manyoni, Singida Dc, Iramba, Ikungi, Itigi, Mkalama na Manispaa ya Singida huku pikipiki 5 zikigawiwa kwa Maafisa Ushirika wa Mkoa huo ambapo zitatumika  kuwafikia wakulima pamoja na vyama vya Ushirika katika kuleta tija kwenye Kilimo.

Aidha Dkt. Mahenge ameeleza kwamba msimu wa kilimo unaokuja Serikali inampango wa kugawa mbegu za alizeti kwa wakulima kama ilivyofanya kwa msimu uliopita hivyo akawaagiza Maafisa Ugani hao kuimarisha usimamizi wa kilimo ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo  ambayo yatachangia pato la wakulima na taifa kwa ujumla.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na Maafisa Ugani, Maafisa Ushirika pamoja na viongozi mbalimbali wa Halmashauri za Mkoa wa Singida wakati wa hafla ya makabidhiano ya pikipiki iliyofanyika nje ya Ofisi ya Mkuu wa MKoa wa Singida

“Niishukuru sana Serikali ya awamu ya Sita kwa jinsi inavyoendelea kutatua changamoto, imeweka msukumo mkubwa kwenye kilimo ili kupata matokeo makubwa, naamini vifaa hivi vitatusaidia kututoa sehemu moja kwenda sehemu nyingine”. RC Mahenge

Amesema, sifa ya mkoa wa Singida ni  kilimo na ufugaji ambapo mazao mbalimbali yanastawi yakiwemo alizeti, pamba, mahindi, vitunguu, parachichi hivyo ujio wa pikipiki  hizo kutasaidia kufanya mapinduzi ya kilimo kwa kuwa wakulima watafikiwa kwa wakati na kupata elimu stahiki alisistiza RC Mahenge.

Hata hivyo RC Mahenge akawaasa Maafisa Ugani hao kutumia vitendea kazi hivyo kwa umakini na  kwa malengo yaliyokusudiwa ili kurejesha thamani yake na kuleta matokea makubwa kwa wananchi huku akionya kutotumika katika biashara binafsi.

Akimalizia hotuba yake akasisitiza maafisa hao kwenda kwenye vyuo vinavyotoa elimu ya udereva ili kuwapata uelewa mpana wa uendeshaji na kuzijua alama za barabarani pamoja na kupata leseni kwa ajili ya usalama wao na chombo husika.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akisisitiza jambo kwa Maafisa Ugani, Maafisa Ushirika pamoja na viongozi mbalimbali wa Halmashauri za Mkoa wakati wa hafla hiyo.  

Naye Natalia  Mosha Afisa Kilimo kutoka Halmashauri ya Singida akiishukuru Serikali kwa kuwapatia pikipiki hizo  huku akiahidi kwamba wataweza kuwafikia na kuwahudumia wakulima wengi kwa muda mfupi jambo ambalo litaleta matokea makubwa katika sekta hiyo.

Baadhi ya Maafisa Ugani pamoja na  Maafisa Ushirika wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge (hayupo pichani) wakati wa hafla hiyo.

Muonekano wa pikipiki hizo.

Mwisho

 

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.