• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

RC Mahenge atembelea Mgodi wa Shanta Gold, awataka Wawekezaji kushirikiana na Serikali

Posted on: January 26th, 2022

Wawekezaji mkoani Singida wametakiwa kushirikiana na Halmashauri za Wilaya wakati wa kuanzisha miradi ya Maendeleo ya Kijamii (Community Socially Responsibility – CSR) ili kukubaliana aina za miradi na namna itakavyotekelezwa lengo likiwa ni kuepuka matumizi makubwa ya fedha kwa kazi ambazo zingetumia fedha kidogo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Satano Mahenge akizungumza wakati wa ziara

Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Satano Mahenge leo January 26, 2022 alipotembelea machimbo ya madini ya dhahabu yanayochimbwa na kampuni ya Shanta Gold iliyopo kijiji cha Mang’onyi wilayani Ikungi ambapo alieleza kwamba miradi yote inayoanzishwa na wawekezaji ipitie katika Halmashauri za Wilaya ambazo zinafahamu mahitaji ya wahusika na  gharama halisi za ujenzi katika maeneo hayo.

Akitolea mfano kwa madarasa yalikamilika hivi karibuni kupitia fedha za uviko 19 RC Mahenge amesema kila darasa liligharimu kiasi cha shilingi milioni 20, ikilinganishwa na madarasa yaliyojengwa na Shanta Gold ambayo yamegharimu Tsh.milioni 28 kwa kila darasa.

“Kama mradi huu mngeshirikisha Halmashauri kwa kiasi kikubwa mngetumia Force Account na mgepata wakandarasi wa bei ndogo na fedha zingebaki zikafanya maendeleo mengine katika jamii. Niwashauri mshirikiane ipasavyo na Halmashauri kupanga aina ya miradi mnayotaka kuipeleka kwa jamii”, alisema Rc Mahenge.

Hata hivyo RC Mahenge akaipongeza Kampuni hiyo ya Shanta Gold kwa kutumia zaidi ya Milioni 190 kwa kupeleka huduma kwa jamii ikiwemo ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na uchimbaji wa visima vya maji huduma ambazo zinafaidisha vijiji vya Mang’onyi, Sambaru, Mlumbi, Tupendane na Mwau.

Aidha, Dkt. Mahenge akaitaka jamii inayozunguka mgodi huo kutumia fursa na kuwa wabunifu kwa kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo ufugaji wa kuku na mama lishe pamoja na kuomba ajira katika kampuni hiyo kwa kuwa kadri mradi unavyokuwa ndivyo mahitaji yatakavyoongezeka.

Meneja wa Mradi Bw. Kundael Mtiro akitoa taairifa ya mgodi kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge mara baada ya kuwasili katika Mgodi huo.

Awali akitoa taairifa ya mgodi Meneja wa Mradi huo Kundael Mtiro amesema mpaka kufikia sasa mradi ulitakiwa kufikia asilimia 46.14 katika utekelezaji wake lakini kwa sababu ambazo zimekuwa nje ya uwezo mpaka sasa utekelezaji wa mradi umefikia asilimia 43.62 .

Hata hivyo Mtiro  akaendelea kufafanua kwamba mpaka June, 2022 mradi utakuwa unakamilisha  robo ya nne ya mwaka ambapo wanategemea kwamba utakuwa umekamilika kwa kuwa tayari washasimika mabomba katika maeno yote yanayohusika pamoja na uchimbaji wa visima, ujenzi wa ofisi na makazi umekamilika kwa asiliami 80.

Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro akizungumza wakati wa ziara hiyo

Naye Mkuu wa Wilaya ya Ikungi Jerry Muro amesema mgodi huo utainua uchumi wa Singida na taifa kwa ujumla ambapo utasisimua sekta nyingine za elimu barabara, zahanati na wananchi kupata ajira.

Amesema Wilaya imeendelea kusimamia hali ya usalama katika eneo la mradi na imehakikisha wanachi wote waliokuwa wanastahili kupata fidia zao wamelipwa kwa wakati.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Ikungi Justice L. Kijazi (katikati) akizungumza wakati wa ziara hiyo . Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Singida na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Ikungi  

Moja ya darasa la Shule ya Msingi lililotembelewa wakati wa ziara hiyo

Mkuu wa Mkoa (waliosimama mbele wa nne kutoka kushoto) akionyeshwa moja ya eneo linalotumika katika  shughuli za machimbo 

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.