• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

RC Serukamba awa mwanasaikolojia katika Mkutano maalumu wa kupitia hoja za CAG Singida DC.

Posted on: June 20th, 2023

Wakurugenzi wa Halmashauri na Wakuu wa Idara wametakiwa kutumia Saikolojia kubwa katika usimamizi na utawala wa watumishi ambao wameonekana kuchelewesha utekelezaji wa majukumu yao ili kutatua changamoto za makusanyo na uzalishaji au ucheleweshaji wa ufungaji wa hoja za ukaguzi (CAG)  zilizopo katika maeneo yao.

Maelekezo hayo yametolewa leo tarehe 20.06.2023 na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba, wakati wa Mkutano maalum wa kupitia hoja za ukaguzi  uliofanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo katika shule ya Sekondari ya Ilongero.

Serukamba ametoa maelezo hayo baada ya kubainika kwamba Afisa Ugavi wa Halmashauri ya Wilaya Singida hakuwa ametekeleza  majukumu yake ipasavyo  hasa katika kusimamia na kutoa  nyaraka muhimu za manunuzi ambazo zingesaidia kufunga hoja za ukaguzi pamoja na kwamba alitakiwa kufanya hivyo katika vikao mbalimbali vilivyopita.

Kutokana na hali hiyo viongozi mbalimbali walilalamikia utendaji kazi wa Afisa Ugavi huyo swala ambalo lilimlazimu RC Serukamba kutoa somo juu ya kushughulika na watu wa namna hiyo ili kazi za Serikali ziendelee wakati ikitafutwa njia mbadala.

Alisema inawezekana  kuna watumishi ambao hawawezi kutimiza majukumu yao mpaka wafuatiliwe kwa ukaribu na baadhi ya wengine wanachangamoto nyingi za kifamilia hivyo ni vyema saikolojia itumike katika kusimamia utendaji kazi wa watu hao.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dkt. Fatma Mganga, amewataka kutembelea Chuo cha Uhasibu cha Mkoani Singida na kuomba wanafunzi wa mazoezi wa gani za ugavi ili kumuongezea nguvu Afisa huyo.

Alisema wakati Serikali inajipanga kuajiri watumishi wapya katika Halmashauri hiyo inaweza kupokea wataalamu wa kujitolea na kuwalipa fedha za kujikimu kupitia mapato ya ndani ili kuepuka kuzalisha hoja katika upande wa manunuzi.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ester Chaula, ameeleza kwamba pamoja na changamoto ambazo zipo bado wanajitahidi kabla ya kufikia tarehe 30 June,  hoja hizo zimefungwa zibaki zile za kisera ambazo zipo nje ya uwezo wao.

Hata hivyo aliendelea kusema kwamba Halmashauri hiyo ilikuwa na hoja 68 lakini zilizofanyiwa kazi ni hoja 36 jambo ambalo waliahidi kuendelea kuzipunguza zaidi.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisisitiza jambo wakati wa kikao hicho.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Singida Ester Chaula, akizungumza wakati wa Mkutano huo.

Mkuu wa Wilaya ya Singida DC Mhandisi Paskas Muragili akizungumza wakati wa Mkutano huo.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Singida Vijijini Eliya Digha, akifunga mkutano huo.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.