• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Serikali kuongeza nguvu matengenezo ya miradi ya TASAF Singida

Posted on: May 27th, 2022

Halmashauri za Mkoa wa Singida ambazo zinapata fedha za miradi ya TASAF zimetakiwa kuiendeleza miradi hiyo kwa kuzifanyia matengenezo na kuiongezea thamani ili iweze kuongeza mapato ya wanufaika na Serikali kwa ujumla.

Miradi hiyo ni kama malambo, Mabwawa na Barabara za kijamii.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge alipotembelea Miradi inayotekelezwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika Wilaya ya Iramba mkoani hapo ambapo alitoa maagizo ya kuendelezwa kwa miradi hiyo kupitia Halmashauri husika ili iweze kuwa na manufaa zaidi kwa wanufaika.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge akizungumza na Wanufaika wa Miradi inayotekelezwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF katika Wilaya ya Iramba mkoani Singida Mei 26, 2022

Aidha akijibu maombi ya wananchi na wanufaika wa Mradi wa bwawa wilayani Iramba ambao waliomba Serikali kusaidia kuongeza kina na upana wa  bwawa hilo, RC Mahenge amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba isaidie matengenezo hayo huku akiwataka kununua vifaranga vya samaki vitakavyofugwa katika bwawa hilo ili liongeze kipato kwao na Serikali kwa ujumla.

Dk. Mahenge ameagiza Maafisa kilimo na mifugo kuhakikisha wanasimamia bwawa hilo ili liweze kuzalisha samaki na liweze kutumika katika Kilimo cha Umwagiliaji wa Mboga mboga na matunda katika eneo hilo.

Katika hatua nyinge RC Mahenge akikagua Ujenzi wa Barabara ya kijamii iliyojengwa na wananchi katika Kijiji cha Misigiri kilichopo kata ya Kiomboi akatumia muda huo kuwaagiza Wakala wa Barabara Vijijini na Mjini TARURA kuongeza kasi katika uwekaji wa madaraja madogo na makubwa katika barabara hiyo ili ziweze kupitika kwa nyakati zote.

Akimalizia ziara yake katika Kijiji cha new Kiomboi RC Mahenge amewataka wanufaika wa TASAF kutumia fedha wanazopata kwa malengo yaliopo ikiwa ni pamoja na kuanzisha miradi midogo midogo itakayosaidia kuendeleza maisha yao huku akiwataka Maafisa wa TASAF ngazi zote kuongeza juhudi za kuelimisha wananchi kuhusiana na mifumo mbalimbali ya mradi ili kupunguza malalamiko ya wananchi.

Katika taarifa yake DC wa Iramba Suleimani Mwenda amesema kwamba TASAF Wilayani hapo inatekelezwa katika vijiji 51 ikiwemo miradi ya uhaulishaji wa fedha, miradi ya muda mfupi kwa walengwa, kuweka akiba na kukuza uchumi wa Kaya kupitia vikundi pamoja na mradi wa Timiza malengo kwa wasichana balehe na wanawake vijana.

DC Suleimani amesema Halmashauri ya Iramba umepokea kiasi cha Sh. Bilioni 1.184 kwa ajili ya kuandaa Mpango wa manunuzi wa vifaa vya ajira za muda kwa walengwa na Mpango wa kunusuru Kaya maskini, malipo ya ruzuku ya uhaulishaji wa fedha kwa Kaya za walengwa na ruzuku ya ajira .

Aidha, DC huyo amebainisha kwamba  vijiji 45 vinatekeleza miradi ya uchimbaji wa malambo wakati vijiji vitano vikitekeleza miradi ya uchimbaji wa Barabara za  jamii na Kijiji kimoja kikitekeleza mradi wa Matenga Maji.

Awali akitoa taarifa  Mratibu wa TASAF Mkoa Patric Kasango amesema Mkoa umepokea jumla ya Tsh. Bilioni 10 kwa ajili ya miradi mbalimbali iliyopo katika Wilaya za Iramba Ikungi Mkalama Manyoni na Singida  ambapo Bilioni 6 kati ya fedha hizo zinatumika kama ruzuku katika masharti ya elimu na Afya.

Baadhi ya Wanufaika wa Miradi inayotekelezwa kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF waliojitokeza wakati wa ziara ya Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt. Binilith Mahenge Wilaya ya Iramba mkoani Singida

RC Mahenge akikagua moja ya Ujenzi wa Barabara ya kijamii iliyojengwa na wananchi katika Kijiji cha Misigiri kilichopo kata ya Kiomboi Wilaya ya Iramba mkoani Singida

Mkuu wa Wilaya ya Iramba Suleimani Mwenda (mwenye suti nyeusi) akisisiza jambo kwa watendaji juu ya usimamizi na utekelezaji wa miradi hiyo wilayani Iramba


Mwisho

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.