• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Serikali Yatakiwa Kuendelea Kutoa Elimu Kwenye Vikundi

Posted on: January 20th, 2022

Wasimamizi wa Vikundi vya Vijana wajasiriamali wadogo wadogo mkoani Singida wametakiwa kuvishauri na kuvisaidia vikundi hivyo kwa kuangalia mipango kazi yao kabla ya kuwakopesha ili fedha watakazozipata waweze kuzitumia vizuri na kuwaletea maendeleo.

Maagizo hayo yametolewa Januari 20, 2022 na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida  Alhaji Juma Kilimba alipokuwa akikagua kikundi cha vijana kilichopo Iguguno katika wilaya ya Mkalama  kinachofahamika kwa jina la Iguguno Youth Group ambacho kinajishughulisha na ufatuaji wa matofali na ufugaji wa kuku wa kienyeji.

Ziara hiyo ya kamati ya siasa imeingia siku ya pili ikiwa na lengo la kukagua miradi iliyojengwa kwa fedha za uviko 19, fedha zitokanazo na tozo za miamala ya simu pamoja na mapato mbalimbali ya Halmashauri.

Aidha Alhaji Kilimba amesema vikundi vyote vinavyokopeshwa fedha za Serikali ni lazima vilelewe vizuri ili vikomae na kufikia kikomo na kupisha vikundi vingine viweze kukua hivyo akawataka Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa na Wilaya kuhakikisha wanawashauri na kuwaongoza hasa katika kipidi wanapowakopesha fedha ili waweze  kufikia malengo yao.

“Ni lazima elimu itolewe kwa wanakikundi wajue namna ya kuandika mahesabu ya mapato na matumizi wapate elimu juu ya namna ya kupambana na majanga yanayoweza kujitokeza katika biashara zao pamoja kuendeleza mitaji  iweze kukua” alisema Bwana Kilimba.

Hata hivyo ameitaka Serikali kuvisaidia vikundi hivyo kupata masoko ya bidhaa wanazozalisha kama sehemu ya kuwaunga mkono hali itakayosaidia kushawishi vijana wengine kujiunga au kuanzisha vikundi mbalimbali vyenye kuongeza ajira na vipato kwa vijana.

Awali akisoma taarifa ya kikundi hicho Bi Winifrida Innocent katibu wa kikundi amesema Halmashauri ya Mkalama iliwakopesha fedha kiasi cha Sh. Milioni 15 ambazo zilitumika kununua baadhi ya vifaa kama mashine ya umeme na inayotumia mikono kwa ajili ya kufyatulia matofali, vibao pamoja na sement.

Aidha ameishukuru Halmashauri ya Mkalama kwa kuwa imekuwa ikiwasaidia ushauri na wataalamu ambao wamekuwa wakiwatembelea mara kwa mara.

Hata hivyo ziara hiyo ya Kamati ya siasa imefanyika katika wilaya mbili za Mkalama pamoja na Iramba ambapo walikagua miradi ya maji, madarasa  na kituo cha afya  ambapo kamati hiyo  imeridhishwa na ujenzi ulivyofanyika na namna ambavyo watoto wamekuwa wakiendelea kusajiliwa katika mashule hayo.

Hata hivyo Mwenyekiti amesisitiza utunzaji wa miradi hiyo ili iweze kusaidia vizazi vijavyo hasa katika vyumba vya madarasa na thamani zake wakati kwenye miradi ya maji akiwataka wataalamu kuhakikisha maji yanasambazwa karibu na makazi ya watu.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.