• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Singida kutatua Mgogoro wa mashamba ya korosho uliodumu kwa miaka mitatu

Posted on: April 23rd, 2022

Kamati zinazoshughulikia changamoto ya ugawaji wa mashamba ya korosho wilayani Manyoni zimepewa Siku Saba kuanza tarehe 25 April 2022  kugawa na kuwaonesha mashamba wakulima wa zao hilo lengo likiwa ni kuhakikisha ifikapo Octoba  2022 yawe yamekwisha safishwa na kilimo kimeanza.

Kauli hiyo imetolewa leo  na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.  Binilith Mahenge alipokutana na wakulima zaidi ya Mia na hamsini  katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya Manyoni waliokuwa wakilalamikia mchakato wa ugawaji wa mashamba kugubikwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kukosa mashamba kwa wakulima waliolipia, mashamba kutosafishwa wakati yalishalipiwa na bàadhi ya wakulima walilipa fedha kwa muda mrefu lakini hawajaoneshwa mashamba yao.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dkt.  Binilith Mahenge akizungumza wakati wa kikao hicho

RC Mahenge ameagiza kamati hizo kutumia Siku Saba kuanzia Siku ya tarehe 25 April kutambua majina ya wote wanaotakiwa kupatiwa mashamba na kuanza kuwaonesha mashamba yao huku akisisitiza kwamba hakuna mtu atakayepoteza haki yake.

Aidha ameagiza kuandaliwa andiko na mihtasari ya mikutano inayofanyika ili kusaidia usimamizi wa mashamba hayo na kurahisisha ufuatiliaji wakati wanapokuja viongozi wapya.

RC Mahenge amesema utaandaliwa utaratibu mzuri wa mawasiliano baina yao na wenye mashamba ili kuondoa changamoto hizo ambazo zimedumu kwa miaka zaidi mitatu.

"Changamoto zote zilizotokea mpaka kusababisha migogoro katika ugawaji wa mashamba na kutuchelewesha  kwa miaka mitatu limesababishwa na ufuatiliaji na usimamizi mbaya uliofanywa na bàadhi ya Maafisa wa Serikali, lazima tutengeneze utaratibu mzuri utakaosaidia kuendeleza zao la korosho mkoani hapa" alibainisha Dk. Mahenge.

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko akizungumza wakati wa kikao hicho.

Kwa upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Singida Dorothy Mwaluko amesema wamedhamiria kuondoa changamoto zilizojitokeza na watahakikisha kwamba ifikapo Oktoba 2022 mashamba yote yatakuwa yamekamilika ili kuongeza uzalishaji wa Korosho na kuongeza mapato ya Wilaya hiyo na Mkoa kwa ujumla.

Hata hivyo RAS huyo amewataka wakulima  kuiamini timu inayoshughulikia matatizo ya  changamoto hizo na kutoa ushirikiano pale utakapohitajika ikiwemo ukaguzi wa nyaraka za malipo na mahitaji mengine.

Aidha kwa kuanza kubadisha utaratibu RAS akabadilisha Mratibu wa Awali na kumteua Bwana Lucas Mkuki Afisa kilimo  kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa kwa ajili ya kuendeleza  uratibu wa ugawaji wa mashamba ambapo atafanya kazi kwa kushirikiana na kamati zitakazokuwepo.

 Akizungumza kwa niaba ya wakulima wengine Abdala Mbonde ameishukuru Serikali ya Mkoa kwa maamuzi yao ya kuhakikisha  changamoto zinatatuliwa na kilimo cha korosho kinaanza.

 

Mbonde ameshauri kamati itakayoundwa ihakikishe haki inatendeka ili wakulima hao waweze kuendelea na uwekezaji huo katika kilimo hicho kwalengo la kujikwamua kiuchumi.

Mkutano ukiendelea

http://singidars.blogspot.com/2022/04/singida-kutatua-mgogoro-wa-mashamba-ya.html


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.