• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Singida Kuvunja Rekodi Ya Uzalishaji Wa Alizeti

Posted on: March 23rd, 2022

Mkoa wa Singida unategemea kuvuna tani 580,000 za alizeti katika msimu wa kilimo wa 2021/22 kulikochagizwa na ukopeshwaji wa  mbegu  zenye ruzuku ya Serikali  kwa wakulima wa zao hilo  ambapo uzalishaji unakadiriwa kuongezeka  zaidi ya  mara tatu  ikilinganishwa na msimu uliopita.

Akitoa kauli hiyo wakati alipotembelea mashamba ya wakulima mbalimbali katika Kata ya Mudida Halmashauri ya Singida Vijijini Mkuu wa mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge amesema wakulima wadogo na wakubwa wameitikia kwa kiasi kikubwa na mbegu walizotumia zimeonesha dalili ya kutoa mavuno mengi.

Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge wakati akisisitiza jambo wakati alipotembelea mashamba ya wakulima mbalimbali katika Kata ya Mudida Halmashauri ya Singida Vijijini Machi 23, 2022

Hata hivyo RC Mahenge amewataka Maafisa Kilimo mkoani hapo kuhakikisha wanaendelea kuwatembelea wakulima na kuwashauri namna ya kutumia dawa kuzuia visumbufu vya mimea vinavoweza kutokea kutokana  na mvua kuendelea kunyesha.

Aidha Dkt. Mahenge akamuagiza  Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na uzalishaji Beatus Choaji kuitisha mkutano wa wadau wa alizeti ili kuanza kutafuta soko la uhakika la wakulima ili wasije kupata hasara wakati wa mavuno.

Hata hivyo Dkt. Mahenge akabainisha kwamba kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa zao la alizeti mkoani hapo kuna kila dalili kwamba uagizaji wa mafuta ya kupikia kutoka nje ya nchi utaanza kupungua kutokana na mavuno yatakayopatikana mkoani hapo.

RC Mahenge akamalizia hotuba yake kwa kuwashukuru wakulima na wadau mbalimbali wa zao la alizeti yakiwemo mashirika na makampuni mbalimbali yaliyojitolea kulima na kuwasaidia wakulima kupata mbegu baada ya ile iliyokuwa inatarajiwa kupitia Wizara ya kilimo kutotosheleza mahitaji.

Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge akionesha moja ya zao la alizeti wakati alipotembelea mashamba ya wakulima mbalimbali katika Kata ya Mudida Halmashauri ya Singida Vijijini 

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya hiyo Mhandisi Paskasi Muragili akafafanua kwamba pamoja na kwamba hawakufikia lengo la upatikanaji wa mbegu kama walivyojiwekea malengo, lakini wananchi na mashirika mbalimbali waliweza kuweka jitihada za upatikanaji wa mbegu kwa kununua sehemu mbalimbali jambo ambalo limesaidia kuongeza uzalishaji na kufanya tuvuke malengo alibanisha Mhandisi Muragili.

“Tokea wananchi wa Singida waanze kulima alizeti hawajawahi kulima mashamba makubwa kwa ufanisi kama kipindi hiki, na hii imetokana na uhamasishaji mkubwa uliofanywa na serikali pamoja na ugawaji wa mbegu kwa mkopo. Singida tutavuna alizeti nyingi kuliko miaka yote” Alibainisha  DC Muragili.

Mkuu wa Wilaya Singida Mhandisi Paskasi Muragili akieleza jambo wakati wa ziara hiyo

Naye Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Beatus Choaji  wakati akitoa taarifa ya kilimo amesema mkoa ulipata  mbegu za alizeti  tani 469 kwa ajili ya kupanda ekari  239,700 jambo ambalo lilitekelezwa.

Bwana Choaji akaendelea kusema kwamba malengo ya mkoa ilikuwa ni kupata mbegu za alizeti tani 581.9 ambazo zingeweza kuwatosheleza wakulima wote na badala yake wakapata kiasi cha tani 469 ambazo hazikuweza kukidhi mahitaji ya wakulima wote.

Amebainisha kwamba wilaya ya Singida Vijijini imepata mbegu  za alizeti tani 76.04 kutoka kwa wakala wa mbegu  nchini ASA  kupitia Wizara ya kilimo ambazo zimesambazwa katika kata 21 za wilaya hiyo.

Hata hivyo Wilaya hiyo ilipata tani 3.8 za alizeti zilizotolewa na shirika la IFARD ili kuwasaidia wakulima wa zao hilo na kuondoa changamoto ya upungufu wa mafuta ya kupikia hapa nchini.

Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Beatus Choaji akitoa taarifa ya kilimo mkoa wa Singida wakati wa ziara hiyo

Akimalizia maelezo yake  Bwana Choaji amemuhakikishia Mkuu wa mkoa huo kwamba kutokana na mwitikio mkubwa wa wakulima pamoja na kwamba walipata mbegu pungufu lakini matokeo yatakuwa makubwa na watakuwa wamevuka malengo ya kiasi walichotegemea kuzalisha.

Awali akitoa taarifa ya wilaya kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Singida Nathalia Mosha ameeleza kwamba Halmashauri hiyo ina eneo linalofaa kwa kilimo lipatalo hekta 321,400  ambapo  3, 400 zinafaa kilimo cha umwagiliaji.

Amesema katika msimu wa kilimo wa 2021/2022 wamelima hekta 38,936 na matarajio ni kuvuna tani 73,936 ambapo mbegu za alizeti zilizotumika ni standard seed, Hysun 33, supersun 66 na recod zilizozalishwa na wakulima wenyewe.

Bi. Nathalia Mosha, akitoa taarifa ya kilimo kwa ngazi ya wilaya kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Singida 

Mkuu wa mkoa Singida Dkt. Binilith Mahenge akisisitiza jambo kwa Maafisa Kilimo mkoa dhidi ya wadudu waharibifu

Ziara ikiendelea

Mwisho.

https://www.blogger.com/blog/post/edit/6903235629886141782/3367812376769514275

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.