Mkoa wa Singida umeendelea kujipambanua kupitia ufugaji wa nyuki shughuli ambayo imekuwa ni kimbilio la watu wengi wanaokwenda kwa lengo la kujifunza kuhusiana na uzalishaji wa asali,nta na mazao mengine mengi yatokanayo na nyuki.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe. Halima Dendego amesema moja ya faida kubwa inayopatikana kupitia nyuki ni upatikanaji wa vumbi la Singida ambalo limekuwa mkombozi kwa wanawake na wanaume kiafya kutokana na kuwa na sifa ya virutubisho vingi kwa wakati mmoja ambavyo huwezi kuvipata kwenye vyakula vingine.
"Unapotumia vumbi la Singida unaenda kupata virutubisho 99 kwa wakati mmoja wengi wanahusisha sana vumbi la singida na kaka zetu lakini hilo ni letu sote wanawake na wanaume."Amesema Mhe. Dendego
Kauli hiyo ameitoa julai 4,2025 Jijini Dodoma alipokuwa akizungumza na wanahabari kuhusiana na mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita Mkoani Singida kwa kipindi cha miaka minne na akieleza kuwa mafanikio waliyopata kupitia ufugaji wa nyuki ni matunda yanayotokanayo na mipango mizuri ya Serikali hasa katika kuendeleza na kuhifadhi misitu.
"Tunayo zaidi ya ekta elfu 4.2 imehifadhiwa, na ndio inatoa fursa ya wafugaji wa nyuki kuweza kufuga nyuki."Amesema Mhe. Dendego
Pamoja na hayo amesema Mkoa umejizatiti kuunga mkono jitihada za Serikali katika kuhakikisha wananchi wanatumia nishati safi ya kupikia hasa kwa kuzingatia kwamba Mkoa huo sio rafiki sana kwenye matumizi ya kuni na mkaa kutokana na mazingira yake.
"Mhe. Rais wetu ni kinara Afrika na sisi tupo naye bega kwa bega,tunahamasisha kupitia mikutano,matamasha,makongamano mbalimbali na wananchi wamehamasika sana." Amesema Mhe. Dendego
Kadhalika,Ameongeza kuwa mpaka sasa Serikali imeshapeleka majiko ya gesi ya kuanzia (30,111) ambayo yanasambazwa vijijini kote.
Akitaja mafanikio mengine amesema katika sekta ya afya Mkoa huo umepiga hatua kubwa katika utoaji wa huduma za afya na sasa wanatoka katika kutoa huduma za afya za kawaida na kuelekea katika utoaji wa huduma za utalii wa tiba.
" tumeweza kujenga zahanati mpya 62,vituo vya afya 22 na hospitali 9." Amesema Mhe. Dendego
SINGIDA
Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA
Telephone: 2502170, 2502089
Mobile: 2502170, 2502089
Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.