• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Taasisi za kifedha za Kanda ya Kati na Mashariki zashauriwa kupunguza riba katika mikopo ya Kilimo

Posted on: March 31st, 2023

Taasisi za kifedha za Kanda ya Kati na mashariki zikiwemo Benki zimeshauriwa kupunguza riba katika mikopo ya Kilimo kufikia asilimia tisa (9) au chini ya hapo ili kuendelea kuwasaidia wakulima waweze kufaidika na mikopo ya Kilimo na shughuli za kilimo kwa ujumla.

Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba,  wakati akifungua Mkutano wa uzinduzi wa kampeni ya kujadili namna ya utunzaji wa mazingira (Kijanisha Maisha) uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kanisa Katoliki uliopo mjini Singida chini ya Shirika la Kilimo la PASS.

RC Serukamba ameeleza kwamba kwa kupunguza riba katika mikopo ya kilimo ni kuunga mkono maagizo ya Rais Samia Suluhu Hassan hadi asilimia tisa hivyo akatumia fursa hiyo kuzipongeza benki ambazo zimefuata agizo hilo.

Aidha Serukamba amewaomba wadau wa kilimo kuendelea kufanya shughuli za uzalishaji kwa kuzingatia kanuni za ukuaji wa kijani shirikishi kama ambavyo PASS Trust wanavyoshauri lengo likiwa ni kuongeza utunzaji wa mazingira na kuzalisha kwa tija.

Hata hivyo RC amelipongeza Shirika la Pass Trust kwa ubunifu ambao wameendelea kuchukua katika kukabiliana na changamoto za wakulima katika mnyororo wa thamani.

Kwa upande wake Kaimu Meneja wa Shirika hilo Herimani Bashiri amesema Shirika limepata mafanikio makubwa kupitia udhamini wanaoufanya katika  miradi ya kilimo ufugaji na misitu pamoja na biashara kupitia mnyororo wa thamani katika kilimo.

Bashiri amesema kwamba Shirika la PASS limetoa ajira kwa watu Milioni 2.7 kati yao wanawake wakiwa ni zaidi ya laki 3.4 na wengi wao wakiwa ni vijana.

Aidha ameeleza kwamba Shirika kwa sasa lina vituo atamizi katika eneo la Chuo Kikuu cha  Kilimo (SUA) Morogoro na Dodoma ambapo vijana wanajifunza mambo mbalimbali ya kilimo ufugaji na misitu.


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.