Mkuu wa Mkoa wa Singida Mhe.Halima Dendego ameshiriki katika ukaguzi wa miradi mbali mbali katika Halmashauri ya Wilaya ya Singida ambayo inategemewa kuzinduliwa na Mwenge wa Uhuru Mkoani Singida ifikapo Julai mwaka huu.Mheshimiwa Dendego Amefanya ukaguzi huo akiambatana na Wajumbe wa kamati ya usalama wa mkoa,Kaimu KatibuTawala wa Mkoa,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Singida,Sekretarieti ya Mkoa,Madiwani,Mwenyekiti wa kijiji,Serikali ya kijiji,Watendaji wa kijiji na wananchi.
Ziara hiyo iliyoanzia katika kijiji cha Pohama, imekagua ujenzi wa Ofisi ya Kijiji cha Pohama mradi wenye gharama ya Shilingi 66,400,000 ambapo shilingi 61,000,000 ni mapato ya ndani huku shilingi 5,400,000 ikiwa ni nguvu za wananchi Ujenzi uliokamilika mwaka 2024 unaosaidia utoaji wa huduma za utawala,kijamii na kiuchumi kwa maendeleo ya wananchi wa ndani na nje ya wilaya ili kudumisha ustawi wa jamii.
Kadhalika ukaguzi umefanyika katika ujenzi wa nyumba ya Waalimu(2 in 1) katika Shule ya Msingi Pohama mradi unaotarajiwa kusaidia waalimu kuishi katika mazingira bora,kuwawezesha kuwa karibu na vituo vyao vya kazi,kuwapunguzia gharama za maisha na kuongeza motisha na usalama wa watumishi.Mradi huu unatekelezwa kwa Shilingi 75,000,000 kwa mapato ya ndani huku 5,000,000/- ikiwa ni nguvu za wananchi.
Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa wa Singida amefanya ukaguzi wa ujenzi wa Kituo cha Afya Ngimu katika Tarafa ya Mgori,Kata ya Ngimu,Kijiji cha Ngimu linalojumuisha ujenzi wa Jengo la wazazi,Jengo la upasuaji,Jengo la Maabara,Jengo la kufulia,vyoo matundu 8,mfumo wa maji taka,kichomea taka,placenta pit,Ash pit,na uwekaji maji safi na umeme.
Awali akisoma taarifa,Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Singida Bi.Ester Chaula amesema Mradi huo unaotarajiwa kukamilika June 2025 unagharimu kiasi cha Shilingi 686,779,126/-ambapo utasaidia kuboresha huduma za afya kwa wananchi wa Halmashauri ya Wilaya wenye uhitaji wa uangalizi na usaidizi maalumu kutoka katika kata ya Ngimu,Itaja na maeneo jirani.
Kadhalika ukaguzi umefanyika katika Shule mpya ya Amali iliyopo katika Tarafa ya Ilongero, Kata ya Msange yenye gharama za Shilingi 544,225,626/-ambayo inatarajiwa kuongeza idadi ya wasomi,na kuongeza ari ya kujiajiri na kuongeza ajira katikabkada ya ualimu endapo ujenzi huo ukikamilika.
Mradi wa maji katika Kijiji cha Kinyamwenda,Tarafa ya Mgori,Kata ya Itaja uliokamilika Julai 2024 ikijumuisha ujenzi wa tangi la kuhuifadhia maji lenye ujazo wa lita 100,000 kwenye mnara wa mita sita wenye gharama ya Shilingi 849,137,591 na tayari mradi huo umekamilika kwa asilimia mia moja.
Mradi huo wa maji unawawezesha wananchi wa Kijiji hicho kupata maji safi na salama ya kutosha katika matumizi ya kawaida na ya kiuchumi kadhalika kupunguza maambukizi ya magonjwa yatokanayo na ukosefu wa maji salama na kuwapatia wananchi muda wa kutosha katika shughuli za kiuchumi ikiwemo kilimo na ufugaji.
Pia ukaguzi umefanyika katika mradi wa ujenzi wa sanduku Kalavati la Mawe katika barabara inayounganisha Sagara-Pohama na Mgori ambapo ujenzi huo wenye gharama ya Shilingi 144,665,670 kutoka mfuko mkuu wa Serikali umewaepusha watumiaji kungojea masaa 2-4 kwa maji ya mvua kupita katika barabara sambamba na kuondokana na tatizo la kukwama na kushindwa kupita kwa watumiaji kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
Mheshimiwa Dendego ametoa maelekezo kwa Uongozi wa Wilaya kuhakikisha wanakamilisha miradi yote kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu ili kuipa thamani fedha na matokeo yanayoonekana katika miradi hiyo.
Kadhalika amesisitiza utunzaji wa mazingira kwa kuhakikisha usafi unazingatiwa katika maeneo yote huku akiwataka wananchi kufika kwa wingi kuupokea mwenge wa Uhuru utakapowadia wilayani hapo kwa lengo la kuzindua miradi mbalimbali itakayoleta tija kubwa kwao.
SINGIDA
Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA
Telephone: 2502170, 2502089
Mobile: 2502170, 2502089
Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.