• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

"USAFI NA USIMAMIZI BORA WA MIUNDOMBINU NI JUKUMU LETU WOTE":RC DENDEGO

Posted on: January 15th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Halima Dendego amewataka viongozi na wakandarasi kusimamia vyema miundombinu ya barabara ili ziweze kuwa bora kwa muda mrefu na zisaidie kukua kwa uchumi wa Mkoa wa Singida huku akiwataka wasimamizi kuwa makini katika utunzaji na usafi wa barabara.

Hayo ameyasema leo (Januari 15,2025) katika kikao cha 48 cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Singida akiwa na wajumbe wa kikao hicho katika ukumbi wa ofisi ya mkuu wa mkoa wa Singida na kuwataka wawe makini wanapoisimamia miradi yote ili kuifanya Singida kuwa sehemu salama na mipango ya kuelekea kuwa jiji.

" Naomba kwa niaba yenu kutoa shukrani za dhati kwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali anayoiongoza ya Awamu ya Sita kwa kutuletea fedha nyingi mwaka uliopita na kutenga fedha nyingi mwaka huu kwa ajili ya matengenezo ya miundombinu ikiwemo barabara, madaraja, vivuko, makaravati ili kuwezesha wananchi wetu kusafiri na kusafirisha mizigo yao kutoka pande zote za Mkoa wa Singida, Hali hii imefanya barabara zetu ziweze kupitika mwaka mzima toka asilimia 78 hadi asilimia 82.8,"  amesema Mhe.Dendego 

Aidha Mhe. Dendego amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2023/2024 Mkoa uliidhinishiwa jumla ya Sh. Bilioni 49.4 ambapo TANROADS Shilingi Bilioni 24.9 na TARURA Shilingi Bilioni 24.5 hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2024 TANROADS walipokea Sh. Bilioni 8.3 na TARURA Sh. Bilioni 12.4 huku mwaka   2024/2025 Mkoa wa Singida umetengewa jumla ya Sh. Bilioni 48.2 ambapo TANROADS wameidhinishiwa Sh. Bilioni 19.1 na TARURA Sh.Bilioni 29.1. 

Katika hatua nyingine Mhe.Dendego ameainisha baadhi ya  kazi kubwa zilizofanyika kwa kipindi cha miaka mitatu  ya Serikali ya Awamu ya Sita ikiwemo kuongeza kilometa za lami kutoka 499.28 hadi 543.09 kwa ongezeko la kilometa 43.81,   Kuongeza kilometa za changarawe kutoka kilometa 1,870.81 mwaka 2021 hadi kilometa 3,118.59 mwaka 2024/2025, Kukamilisha ujenzi wa madaraja makubwa 27, madogo 1,638, culverts 2,341 na vivuko 65.

 Katika kuhakikisha miradi  ya maendeleo inaendelea kudumu kwa muda mrefu Mheshimiwa Dendego amesema kuwa kila mmoja ana wajibu wa kuilinda na kuiheshimu huku  akiwaelekeza wanaosimamia usafi hususani katika Halmashauri ya Manispaa ya Singida kudhibiti watu ambao wamekuwa wakitupa takataka kwenye mitaro hali ambayo inasababisha mji kuwa mchafu.

" Wajibu wetu mkubwa ni kulinda miundombinu hiyo na kuhakikisha muda wote panapotokea          uharibifu   kwa  sababu yeyote ile tunafanya matengenezo mara moja. Na iwapo uharibifu huo utasababishwa na uzembe au matendo yasiyofaa ya binadamu kama, Kung’oa vyuma,  Kumwaga mafuta barabarani,  Ajali za kizembe,   Kupitisha mifugo na nyinginezo hatua kali zichukuliwe dhidi ya waharibifu hao," Dendego

Naye Meneja wa TANROADS Mkoa wa Singida, Mhandisi Msama Msama,akisoma taarifa ya utekelezaji wa miradi,ameainisha miradi mbali mbali ya ujenzi wa bara bara kitaifa, utekelezaji wa kikazi na kifedha, manunuzi ya kazi za matengenezo ya barabara kwa mwaka 2023/2024 ambapo jumla ya mikataba 43 yenye thamani ya shilingi 16,435,498 sawa na asilimia mia moja ilisainiwa.

 Amesema kuwa  katika kudhibiti ajali ambazo zimekuwa zikitokea eneo la mlima sekenke barabara kuu ya Singida-Mwanza wameomba fedha Benki Kuu ambayo imeahidi kutoa ili upanuzi wa barabara eneo hilo uweze kufanyika.

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Katibu wa CCM Mkoa, Katibu Tawala wa Mkoa, Wakuu wa Wilaya,Waheshimiwa Wabunge;Wenyeviti wa Halmashauri,Meneja wa TANROADS Mkoa,Meneja  wa TARURA Mkoa,Wakurugenzi wa Halmashauri za Wilaya,Wawakilishi toka Sekta Binafsi na Wahandisi



@USIKOSE KUFUATILIA MITANDAO YETU YA KIJAMII

INSTAGRAM:SINGIDA RS

FACEBOOK:SINGIDA RS

YOUTUBE:RAS SINGIDA 


Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.