• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

VETA Watakiwa Kuhamasisha vijana wa Sekondari kujifunza ufundi.

Posted on: February 28th, 2023

Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA ) wameshauriwa kuimarisha mifumo kuanzia chini kueleza umuhimu wa ufundi na faida zake ili kuwavutia vijana wengi kujiunga katika vyuo hivyo.

Ushauri huo umetolewa leo na Katibu Mkuu CCM Taifa Daniel Chongolo, alipotembelea ujenzi wa majengo ya Chuo cha VETA Ikungi na kusihi kutengeneza programu ya kueleza umuhimu wa ufundi na faida zake ili kuongeza kipato na kuimarisha dhana ya ujasiriamali.

Amesema kwa sasa Taifa lina vyuo vichache vya Serikali ambavyo vinatoa elimu ya kati hivyo kusababisha watumishi kwenye mashirika mbalimbali kushindwa kusimamia upatikanaji wa uzoefu kazini.

Chongolo alisema tunaweza kuwa na vyuo vingi vya VETA lakini usipowekwa mfumo mzuri wa kuwafanya vijana waone umuhimu wa kujiunga na vyuo hivyo tutajikuta tunabaki na majengo tu ambayo hayawanufaishi wananchi.

"Anzeni kutengeneza programu ya kwenda chini kwenye shule za Sekondari ili kabla vijana hawajamaliza kueleza umuhimu wa ufundi, faida zake na namna unavyoweza kuzifikia faida hizo," alisema.

Alisema Serikali katika miaka hiyo mitatu imekuwa ikitoa fursa ya mafunzo ya ufundi bure lakini jambo la msingi ni VETA kupata vijana wa kutosha wanaojiunga na vyuo hivyo.

Naye Mkurugenzi wa VETA Kanda ya Kati, John Mwanja, alisema ujenzi wa chuo cha VETA Ikungi ulianza katika bajeti ya 2019/2020 ambapo hadi sasa Sh. Bilioni 2.3 zimeshatumika katika ujenzi huo ambao utakamilika Aprili mwaka huu.

Mwanja alisema ili chuo hicho kiweze kuanza kazi kwa ajili ya kukamilisha ujenzi, Serikali imetoa Sh. Milioni 259 na kwamba kitakapoanza kitaanza kutoa mafunzo ya kozi ndefu kwa wanafunzi 240 na wa kozi fupi kati wanafunzi 250 hadi 900 kwa mwaka.

Mwisho

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.