• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Viongozi wa dini mkoani Singida waombwa kusaidia kutoa elimu ya Lishe katika Nyumba za Ibada

Posted on: April 3rd, 2022

Viongozi wa dini mkoani Singida wameombwa kuisaidia jamii ya maeneo hayo kwa kutoa elimu ya Lishe katika Nyumba za Ibada  kwa watoto na mama wajawazito ili kupunguza tatizo la utapia mlo ambalo limekuwa likiwaathiri watoto wa umri wa chini ya miaka mitano kwa kiasi kikubwa mkoani hapo.

Akizungumza katika kikao kazi kilichofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa  huo Kaimu Afisa Tawala Mkoa Beatusi Choaji amesema elimu kuhusu Lishe bado haijatolewa kwa kiasi cha kutosha na maana bado jamii inaathirika na swala la kuacha kula makundi muhimu ya vyakula, hivyo kuwaomba viongozi wa dini kusaidia kutoa elimu hiyo ili kubadilisha  Tabia ya ulaji kwa wananchi hao.

Kaimu RAS huyo amesema kwamba wakulima wa Mkoa wa Singida wanalima vyakula vingi vikiwemo viazi lishe  mahindi maharage na wanaongoza kwa ufugaji wa kuku wa kienyeji hivyo utapia mlo kwa kiasi kikubwa linaweza kusababishwa na kutowalisha vizuri watoto vyakula na sio kwamba hakuna vyakula.

Amewataka wataalamu wa Lishe mkoani hapo kutumia majukwaa mbalimbali kupeleka elimu ya Lishe kwa wananchi na kuhakikisha  katika Zahanati na vituo vya Afya wanakuwa na utaratibu wa kutoa elimu ya Lishe kwa kuwafuata watu majumbani na sio kuwasubiri Hospitalini wakiwa tayari wameshaathirika.

Akimalizia Kikao hicho Kaimu Katibu Tawala Mkoa akaagiza kuwakutanisha  Maafisa Lishe wa ngazi zote za Wilaya na Halmashauri ili kuja na mikakati mipya ya kupambana na tatizo la Lishe pamoja na kuwekana sawa kwenye zoezi uchukuaji wa takwimu za hatua za mapambano kwenye kutenga na kutumia bajeti zinazotengwa katika Halmashauri hizo.

Mganga Mkuu wa Mkoa Singida (wa kwanza kushoto) Victorine Ludovick, akisoma taarifa ya Lishe wakati wa kikao hicho

Naye Mganga Mkuu wa Mkoa huo Victorine Ludovick akabainisha kwamba bado changamoto ya umbali kutoka vituo vya Afya na makazi ya wananchi imeonekana kuwa changamoto kwa kuwa wagonjwa wengi wanashindwa kufika vituo vya huduma kwa sababu ya umbali huo.

Hata hivyo amesisitiza kuchukua hatua za  kuongeza mbinu za uelimishaji kwa Jamii ili kuweza kutumia vyakula vinavyopatikana katika maeneo yao na kusaidia kukinga uwepo wa utapia mlo badala ya kujikita katika kutibu.

Kikao hicho kiliwahusisha wataalamu wa Lishe kutoka Sekta binafsi, Sekretarieti ya Mkoa, wawakilishi wa vyombo vya habari na viongozi wa dini.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.