• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

*WAJASIRIAMALI WADOGO WADOGO KUNUFAIKA NA VITAMBULISHO VYA KIDIJITALI.

Posted on: December 5th, 2024

Mkuu wa Wilaya ya Singida Godwin Gondwe leo Disemba 05,2024 amemuwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Singida Halima Dendego katika uzinduzi wa zoezi la ugawaji wa vitambulisho vya kidijitali kwa wajasiriamali wadogo wadogo mkoani Singida ambao umefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Singida.

Uzinduzi huo umehudhuriwa  na viongozi na wawakilishi mbalimbali akiwemo Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya viwanda na biashara, Maafisa maendeleo ya jamii kutoka ngazi za Mkoa na  halmashauri ambao ni waratibu wa dawati la wafanyabiashara ndogo ndogo,Viongozi wa Wafanyabiashara ndogo ndogo(wajasiriamali) na wawakilishi kadhaa wa wafanyabiashara ndogo ndogo.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo Mkuu wa Wilaya  amesema ni wakati sasa wa wajasiriamali kwenda kunufaika na fursa mbali mbali kutokana na kupata vitambulisho hivyo huku akitoa agizo Kwa waratibu wa zoezi hilo wilaya zote  kuongeza kasi ya kuandikisha wajasiriamali hao ili wengi waweze kunufaika.

“Shughuli ya uzinduzi na ugawaji wa vitambulisho vya kidigitali kwa ajili ya Wafanyabiashara ndogondogo katika Mkoa wa Singida umetokana na changamoto ya muda mrefu ya kutaka kuwatambua wafanyabiashara ndogondogo nchini kwa idadi yao na umuhimu wa kuweka utaratibu mzuri wa kuwaratibu ili waweze kukua katika shughuli zao za kiuchumi na kijamii Kwa lengo la  kuwainua wafanyabiashara hao kiuchumi na kijamii pamoja na utayari wa kuhakikisha kuwa changamoto zao zinapatiwa ufumbuzi na wataalam kwa wakati”. Amesema DC Gondwe.

Awali,Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya viwanda na biashara,Bi.Donatila Vedasto ameainisha makundi ya Wafanyabiashara ndogondogo,

"Wafanyabiashara ndogondogo nchini tunazingatia biashara zote halali zinazofanywa na wafanyabiashara hao ambazo zinatambuliwa na Mamlaka. Aidha, wafanyabiashara ndogondogo wanajumuisha machinga, mama na baba lishe, madereva wa bodaboda na bajaji, wasusi, vinyozi, wakulima wa bustani ndogondogo na wauzaji wa vyakula kama vile matunda na mbogamboga. Kwa ujumla sekta hii inachangia kwa kiwango kikubwa kutoa ajira kwa vijana wanaohitimu katika ngazi mbalimbali za elimu na taaluma hapa nchini”. Alisema Bi.Donatila

Wema Yona mfanyabiashara ambaye amepata kitambulisho siku ya Leo,amesema anategemea kupata fursa nyingi zaidi kupitia vitambulisho hivyo vya wafanyabiashara ndogo ndogo ikiwemo fursa za kupata mikopo ambazo walikua hawazipati ,akisema kuwa sasa watafanya kazi kwa kujiamini zaidi huku akitoa wito kwa wajasiriamali wote kupata vitambulisho hivyo ili kuwa karibu na fursa.

Pia,ameomba ushirikiano wa kutosha kutoka kwa viongozi uendelee ili kuweza kuzitatua changamoto zitakazojitokeza kwa lengo la kukuza uchumi wa wajasiriamali mmoja mmoja na Singida kwa ujumla kwa kuongeza mapato kutokana na kulipa kodi.

Mpaka sasa takribani wajasiriamali  894 wameshasajiliwa na kupata vitambulisho hivyo Mkoani Singida.



Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.