• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Wakufunzi City Collage waamka kudai Haki zao, RC Mahenge akipa Muda kujipanga kabla Sheria haijachukua mkondo wake.

Posted on: June 4th, 2022

Vyuo vya Kati vya binafsi vilivyopo Mkoa wa Singida vimetakiwa kufuata taratibu Kanuni na Sheria walizopewa wakati wa usajili ili kuondoa migogoro inayojitokeza baina yao na Watumishi ili kutoa huduma nzuri kwa wanafunzi wanaolipia fedha zao na wakufunzi wanaotoa huduma hiyo.

Kauli hiyo imetolewa hivi karibuni na Mkuu wa Mkoa huo Dkt. Binilith Mahenge alipotembelea chuo cha City Collage kilichopo maeneo ya Mwenge Mkoani hapo ambacho kimekuwa na Migogoro baina ya viongozi na Watumishi wake kwa kile kilichoelezwa kwamba ni kufanya kazi bila ya kuwa na mikataba ya kazi, kucheleweshewa mishahara yao na kutofuatwa kwa taratibu za ajira baina yao na wamiliki wa Chuo hicho.

Akiongea baada ya kupokea taarifa ya chuo hicho RC Mahenge ametoa maagizo kwa Mkuu wa chuo na Meneja kumletea ofisini kwake  taarifa iliyokamilika inayoonesha miongozo waliyopewa na namna wanavyoitekeleza, na pia ioneshe makubaliano baina yao na PSF kwa ajili ya malimbikizo ya Pensheni, mikataba ya wafanyakazi na namna ambavyo wamejipanga kuondoa changamoto zilizopo chuoni hapo.

Hata hivyo Mahenge amesema ni lazima chuo hicho kiwe na Bodi ambayo itafanya kazi ambayo itasaidia kuondoa changamoto za watumishi na kuleta ushindani kwa kutoa huduma bora, huku akiwataka kuhakikisha wanakuwa na mfumo mzuri wa ajira kwa watumishi wake na kufuata taratibu zote za kiutumishi.

Aidha amekemea vikali tabia ya viongozi hao kuwatishia watumishi kuwafukuza kazi pindi wanapodai haki zao na kuwataka kufahamu kwamba madai hayo ni haki ya mtumishi hivyo kuwataka kufanya mabadiliko kabla Sheria haijachukua mkondo wake.

Akitoa taarifa ya chuo hicho Mkuu wa Chuo ambaye jina lake halikuweza kufahamika mara moja  alisema chuo kina jumla ya wanafunzi 112 na watumishi 10 ambapo wanaume ni wanane (8) na wanawake ni wawili (2) na malipo ya Ada kwa kila Mwanafunzi yakitajwa kuwa ni wastani wa  Tsh laki nane (800,000/=) kwa kila Mwanafunzi.

Mkuu wa Chuo huyo anasema baadhi ya walimu wana mikataba na wengine hawana kwa kuwa bado ofisi ya Meneja inaendelea na michakato ya kuwapatia walimu waliobaki mikataba jambo ambalo lilipingwa vikali na wakufunzi wakidai mikataba hiyo imejazwa jana baada ya kusikia ujio wa Mkuu wa Mkoa.

Wakufunzi hao wamedai kufanya kazi kwa miezi minne (4) bila malipo na waliojaliwa kulipwa walikadiriwa kiasi cha kuwalipa jambo ambalo limesabisha maisha kuwa magumu huku wakipata vitisho kupitia mkuu wa shule kusimamishwa kazi kutokana na malalamiko yao kwenda Serikalini waliendelea kueleza wakufunzi hao.

Kwa upande wake kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Singida Jeshi Lupembe amesema kwamba chuo hicho bado kina nafasi ya kuonana na wataalamu wa Serikali katika Manispaa hiyo ili kuweza kupata miongozo mbalimbali ya kuendesha vyuo kama hivyo.

Jeshi amesistiza kufuatwa kwa taratibu hizo kwakuwa wanaoumia ni wananchi ambao watoto wao wanapata elimu isiyokidhi na kupewa vyeti visivyostahili hivyo kushindwa kuingia katika ushindani na wahitimu kutoka vyuo vingine.

Chuo hicho kinatoa kozi za TEHAMA, Malezi ya Watoto, Ufundi magari, Udereva, Utalii na Hotelia.

Kikao hicho kilihudhuriwa na wataalamu wa Halmashauri, Maafisa kazi, Wataalamu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa Chuo cha vyeta Singida na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa.

Mwisho

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.