• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

WAKULIMA WA CHIKUYU-MANYONI WAMPONGEZA RAIS SAMIA KWA MIRADI YA UMWAGILIAJI

Posted on: October 4th, 2022

Wakulima wa maeneo ya Chikuyu, Maweni na Kintinku wilayani Manyoni mkoani Singida wamempongeza Rais Samia Suluhu Hassan na Serikali ya awamu ya sita kupitia Wizara ya Kilimo kwa mikakati ya ujenzi wa miradi mipya ya umwagiliaji na ukarabati wa miradi ya zamani katika wilaya ya Manyoni.

Hayo yamesemwa leo wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Kilimo Mhe. Anthony Mavunde katika miradi ya umwagiliaji za Chikuyu, Ntambaliza, Ngaiti na Udimaa ambapo amepata nafasi ya kukagua skimu hizo pamoja na kuongea na wakulima kuwahakikishia azma ya Serikali kuona skimu zote hizo zinafanya kazi ili kuongeza uzalishaji wa mazao ya kilimo na kukuza uchumi wa wakulima.

“Mhe. Rais Samia anayo dhamira kubwa ya kumuona mkulima wa Tanzania ananufaika na kilimo chake kwa kulima kwa tija na kuongeza kipato kupitia kilimo cha uhakika cha umwagiliaji.

Mhe. Rais ameelekeza eneo la Mbwasa wilayani Manyoni kujengwa bwawa lenye thamani ya Tsh. 20 bilioni lenye uwezo wa uhifadhi maji wa mita za ujazo Milioni kumi pamoja na skimu za umwagiliaji katika eneo hilo.

“Na mimi namuagiza Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji kusimamia ukarabati wa kingo za mto za mradi wa umwagiliaji Chikuyu sambamba na kufanya usanifu wa miradi ya Ntambaliza, Udimaa na Ngaiti ili kuwa na chanzo cha uhakika cha maji na miundombinu ya mifereji ya maji ya umwagiliaji”. Alisema Mavunde

Akitoa ufafanuzi wa baadhi ya mambo yaliyojitokeza, Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji Ndg. Raymond Mndolwa amesema kwamba Tume imejipanga kuhakikisha miradi yote mipya ya skimu za umwagiliaji inakuwa na chanzo cha uhakika cha maji ili kuruhusu shughuli za kilimo cha umwagiliaji kufanyika zaidi ya mara moja kwa mwaka.

Naye Mbunge wa Jimbo la Manyoni Mashariki Mhe. Dr. Pius Chaya kwa niaba ya wakulima wote amempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wizara ya Kilimo kwa kazi kubwa ya miradi ya umwagiliaji inayofanyika katika Wilaya ya Manyoni ambapo kupitia miradi hiyo wananchi wa maeneo hayo watakuza vipato vyao na kutatua changamoto kubwa ya ajira hususani kwa vijana.

Mkuu wa Wilaya ya Iramba ambaye anakaimu Wilaya ya Manyoni kwa sasa Mhe. Suleiman Mwenda ameahidi kwa niaba ya Serikali ya Wilaya kusimamia utekelezaji wa miradi hii kwa uadilifu na umakini mkubwa ili ilete matokeo chanya kwa wakulima wa mpunga wa skimu hizo.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.