• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

WATAALAM WALIOPATA MAFUNZO YA CHANJO YA UVIKO 19 WATAKIWA KUPELEKA ELIMU KWA JAMII

Posted on: September 24th, 2021

Mafunzo ya wataalamu wa afya  na viongozi mbalimbali wametakiwa kusambaza elimu ya chanjo ya UVIKO 19 katika vituo mbalimbali vinavyotoa chanjo  na kwenye mikusanyiko ya watu ili kusaidia kupunguza athari  za ugonjwa huo.

Akizungumza leo wakati wa kufunga mafunzo ya Siku mbili yaliyofanyika mkoani Singida na kuwahusisha Waganga wakuu wa Wilaya,  Maafisa habari  na baadhi ya wawakilishi kutoka wizara mbalimbali, Mganga Mkuu wa Mkoa, Victorin Ludovick amesema  kumalizika kwa mafunzo hayo ndio mwanzo wa kutoa elimu kwa watoa chanjo na wananchi kwa ujumla.

Amesema elimu waliyopata wakufunzi hao wataenda kuwafundisha wengine kuanzia ngazi ya Halmashauri mpaka Vijijini

Mganga Mkuu Mkoa wa Singida, Victorin Ludovick akisisitiza jambo wakati wa mafunzo. (Katika) Mwakilishi wa Ofisi ya Rais -  TAMISEMI, Dinah Atinda na (kulia) Mshauri wa Ugavi kutoka shirika la JSI wanaoshirikiana na wizara ya Afya kupitia idara ya chanjo.  

Dkt.Ludovick amesema elimu  waliyopata imetoa muongozo wa  utoaji wa elimu  sehemu mbalimbali ikiwemo minadani na kwenye masoko na sehemu zenye watu wengi.

Mafunzo yamefanya zoezi la utoaji wa elimu ya chanjo  kuwa jepesi kwakuwa wataalamu wengi walishapata uzoefu mkubwa kwenye mambo ya utoaji wa chanzo. Alisema Mganga Mkuu wa Serikali.

"Mazoezi kama haya tushayafanya sana kwa hiyo naamini tunaenda kutekeleza tulichojifunza na nategemea kuona matokeo makubwa" alisistiza Dkt. Ludovick.

Pamoja na mafunzo hayo Dkt Victorine amesema mafunzo hayo yatumike  kubuni njia mbadala ya kuwafikia wananchi ili kuwaelimisha na kuhamasisha chanjo kwa kila mtu.

Amebainisha kwamba njia nyingine ni kuwatumia  viongozi wa dini ili wafikishe ujumbe kwa waumini wao juu ya umujimu wa kupata chanjo na kuondoa imani potofu kwa jamii dhidi ya chanjo ya UVIKO 19

Mwakilishi wa OR -  TAMISEMI, Dinah Atinda  akisisitiza jambo wakati wa mafunzo

Awali Mwakilishi wa Ofisi ya Rais -  TAMISEMI, Dinah Atinda  amesisitiza kuwa mafunzo hayo yanalenga kuwajengea uwezo watoa huduma za afya na pia viongozi na watu maarufu katika jamii husika ili waweze kuelimisha na kuhamasisha wananchi juu ya UVIKO-19 .

Amesema Mpango Jamii Shirikishi na Harakishi wa Chanjo dhidi ya UVIKO-19 umeandaliwa na Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  kwa kushirikiana na OR - TAMISEMI  na unaendelea kutekelezwa nchi nzima.

Hata hivyo amebainisha lengo la mafunzo hayo kuwa ni  kuwajengea uwezo watoa huduma za afya , viongozi na watu maarufu katika jamii husika ili  kuelimisha na kuhamasisha wananchi kuendelea kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa UVIKO-19 na kupata chanjo dhidi ya ugonjwa huu.

Mafunzo yakiendelea, kulia ni Mganga Mkuu wa Mkoa Singida Victorin Ludovick

Afisa Mpango wa Chanjo kutoka Wizara ya Afya - TAMISEMI, Mpango wa Taifa wa chanjo akizungumza wakati wa mafunzo hayo. 

 Viongozi mbalimbali wa Serikali na Maafisa Watendaji (walio kaa) wakiwa katika picha ya pamoja na timu ya uendeshaji na usimamizi wa huduma za afya mkoa wa Singida muda mfupi baada ya kumaliza mafunzo kuhusu Mpango Shirikishi na Harakishi wa Chanjo ya UVIKO 19 kwa wakufunzi na wadau wa afya mkoani Singida. Septemba 23 - 24/2021 

Kwa habari picha zaidi bonyeza singidars.blogspot.com

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.