• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

Wazazi watakiwa kuwa waangalifu kwa watoto katika kipindi hiki cha mvua

Posted on: February 15th, 2022

Wazazi na walezi Mkoani Singida wametakiwa kuchukua tahadhari katika kipindi hiki cha mvua dhidi ya uwepo wa madimbwi, mifereji kujaa maji pamoja na vyoo vya mashimo kwa kuwa imeonekana kuwa hatari kwa watoto.

Wito huo umetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilithy Mahenge leo Februari 15, 2022 alipofanya ziara katika shule ya msingi Mndimu iliyoko wilayani Ikungi Mkoani hapa.

Mkuu wa Mkoa wa SIngida Dk. Binilithy Mahenge akiongea wakati alipofanya ziara katika shule hiyo.

Amesema katika kipindi hiki cha mvua kila mzazi au mlezi anapaswa kuangalia miundombinu yote ya barabara na majumbani mwao kama sehemu ya kuchukua tahadhari na kuepuka maafa yanayoweza kutokea kutokana na uwepo wa mvua nyingi.

Hata hivyo amebainisha kwamba katika kipindi hiki cha mvua kuna uwezekano mkubwa wa majengo na miundombinu mbalimbali kupata nyufa ambazo zinaweza kusababisha majanga hivyo ni jukumu la kila mmoja kuchukua tahadhari.

RC Mahenge akawaagiza Wahandisi mkoani hapo kutembelea na kukagua maeneo yote na kufanya tathmini itakayoonesha uharibifu wa miundombinu ya shule madaraja na barabara kama sehemu ya kuepusha majanga katika jamii inayowazunguka.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji Halmashauri ya wilaya Ikungi Justice Kijazi akatumia muda huo kumueleza Mkuu wa mkoa kwamba kutokana na uwepo wa mvua nyingi ipo miundo mbinu ya baadhi ya shule ikiwemo shule ya msingi Mandimu ambayo imeathiriwa na mvua zinazoenedelea kunyesha.

Kijazi akaendelea kufafanua kwamba tayari Serikiali imetoa jumla ya Tsh. Milioni 40 na wakati huo Mbunge wa jimbo la Ikungi Mashariki akatoa ahadi ya Tsh.  milioni moja kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa katika shule hiyo ambapo RC Mahenge naye akaahidi kutoa kiasi cha Tsh. Milioni moja kwa ajili ya ujenzi huo.

Wakati huo huo RC. Mahenge ametoa pole kwa familia ya watu sita (6) wa Kata ya Ihanja wilayani humo ambao wamelazwa katika kituo cha afya cha Ihanja baada ya kula uyoga ambao umeonekana kuwa na sumu na kuathiri afya zao.

Amesema familia hiyo inahusisha watoto wane (4) na wazazi wawili (2) ambao hivi karibuni walikula uyoga huo kwa kuchanganya na mboga za majani kama sehemu ya kitoweo pasipo kujua kama ungekuwa na sumu.

Aidha RC Mahenge amewataka wataalum wa afya na maafisa kilimo kutoa elimu kuhusu aina za uyoga na matumizi yake ili kuondoa changamoto za kiafya.



Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • UKAGUZI MIRADI SINGIDA DC,MHE DENDEGO ATOA MAAGIZO

    May 13, 2025
  • KAMATI YA LISHE YAJA NA MIPANGO KABAMBE YA UTEKELEZAJI SINGIDA

    May 12, 2025
  • HUDUMA ZA KIBINGWA ZAWAFIKIA WAGONJWA ZAIDI YA 3000 SINGIDA.

    May 09, 2025
  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.