• Contact Us |
    • Complaints |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Blog |
Singida Regional Website

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government Singida Regional Website

  • Home
  • About Us
    • History
    • Vision and Mission
    • Regional Leaders
  • Administration
    • Regional Secretariet Structure
    • Sections
      • Administration and Human Resources
      • Planning and Coordination
      • Economy and Production
      • Infrustructure
      • Local Government
      • Health
      • Education
      • Water
    • Units
      • Finance and Accounts
      • Internal Audit
      • Information and Communication Technology
      • Legal Services
      • Procurement and Supply
  • Districts
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • LGA
    • Ikungi DC
    • Iramba DC
    • Itigi DC
    • Manyoni DC
    • Mkalama DC
    • Singida DC
    • Singida MC
  • Investiment Opportunity
    • Agriculture
    • Livestock
    • Industries and Trade
    • Mining
  • Our Services
    • Health
      • Medical Specialists
      • Clinical Services
      • Preventive Care
      • Social Welfare
      • Environmental Health
      • Nutrition
    • Education
    • Water
    • Agriculture
  • Publications
    • Bylaw
    • Customer Service Charter
    • Strategic Plan
    • Reports
    • Forms
    • Guidelines
    • Investment Guide
  • Media Center
    • Gallery
    • Videos
    • Speeches
    • Press Release

WAZEE MKALAMA WAPATIWA KADI ZA MATIBABU BILA MALIPO

Posted on: June 15th, 2025

Jumla ya wazee 20 kutoka Wilaya ya Mkalama wamekabidhiwa kadi za msamaha wa matibabu bure wakati wa Maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili kwa Wazee Duniani kwa Mkoa wa Singida, yaliyofanyika Juni 15,2025 katika ukumbi wa Sheketela uliopo  Halmashauri ya Wilaya ya Mkalama.

Akizungumza katika hafla hiyo kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Mhe. Moses Machali, aliwataka wazee kuwa mfano wa kuigwa katika jamii kwa kusimamia maadili na malezi bora ya watoto, pamoja na kupaza sauti dhidi ya vitendo vya ukatili ndani ya familia na jamii kwa ujumla.

“Tunayoyaona leo ni matokeo ya malezi yetu. Tulishindwa kuwasimamia watoto wetu vizuri, matokeo yake tunaona baadhi ya watoto wamewatelekeza wazee wao,” alisema Mhe. Machali.“Nitumie nafasi hii kuwahimiza wazee kuwasimamia watoto wao wenye watoto katika malezi, ili tuepukane na changamoto kama hii.”

Mhe. Machali aliwakumbusha wazee kutumia ofisi za Ustawi wa Jamii zilizopo katika halmashauri zao kama njia rasmi ya kuripoti vitendo vya unyanyasaji na ukatili wanavyofanyiwa, badala ya kuvumilia kimya kimya hali zinazowakandamiza.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Wazee Mkoa wa Singida, Mchungaji Mbura Joel, alitoa pongezi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zinazofanyika katika kulinda haki na ustawi wa wazee nchini.

Akizungumza kuhusu kadi hizo za msamaha wa matibabu, Afisa Ustawi wa Jamii Wilaya ya Mkalama, Bi Mwajuma Yusuphu, alisema kuwa kadi 20 zilizotolewa leo ni sehemu ya jumla ya kadi 5,000 zilizotolewa kwa wazee mbalimbali wilayani humo kuanzia Julai 1, 2024 hadi Juni 2025.

Maadhimisho hayo yalilenga kuhamasisha jamii kutambua, kulinda na kutetea haki za wazee sambamba na kuhakikisha kuwa kundi hilo linaishi kwa heshima, usalama na upendo katika familia na jamii.

Announcements

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • View All

Latest News

  • MAAFISA MAENDELEO KIKAANGONI,WAASWA KUJIPIMA KWA MATOKEO NA SIO IDADI YA VIKAO.

    June 30, 2025
  • HAPO AWALI NA SASA KATIKA MIUNDOMBINU YA ELIMU SINGIDA

    June 27, 2025
  • MIRADI MBALI MBALI YA UJENZI INAYOENDELEA MKOANI SINGIDA

    June 27, 2025
  • WENYE MAHITAJI MAALUM SINGIDA WASHIKWA MKONO

    June 25, 2025
  • View All

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
More Videos

Quick Links

  • Press Release
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • SINGIDA RS PROCUREMENT NOTICE
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Related Links

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    SINGIDA

    Postal Address: P O BOX 5 SINGIDA

    Telephone: 2502170, 2502089

    Mobile: 2502170, 2502089

    Email: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap
    • Service

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.