Halmashauri zenye mbegu za ruzuku za Alizeti ambazo hawazitumii zimeelekezwa kuhamishiwa katika Halmashauri zenye uhitaji ili wakulima waendelee kuzitumia hasa katika kipindi hiki ambacho mvua zinaendelea kunyesha.
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba ametoa ufafanuzi huo leo katika Kikao cha Kamati ya Ushauri ya Mkoa ambayo imekutana katika ukumbi wa Mkutano wa Ofisi hizo baada ya Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Uchumi na Uzalishaji Selastian Beatus Choaji kueleza kwamba zipo Halmashauri ambazo walipata mbegu za ruzuku za alizeti ambazo hazikutumika.
Serukamba alitoa maelekezo kwamba kila Halmashauri ilitoa mahitaji yake ya mbegu hivyo ulipata kulingana na uhitaji wake hivyo kama Halmashauri imeona haiwezi kutumia mbegu hizo izipeleke katika Halmashauri zote uhitaji vinginevyo watazilipa.
"Singida tumepata mbegu hizi zenye ruzuku ya Serikali ki mkakati hivyo hayupo tayari kuona zikiacha kufanyiwa kazi iliyotegemewa, Mkurugenzi atakaye baki na mbegu hizi lazima alipe" Alisema Serukamba.
Aidha ametoa onyo kwa Maafisa kilimo na watendaji wa Vijiji ambao wamekaa na mbegu ofisini wakati wakulima wakiwa wanazihitaji jambo ambalo RC Serukamba amesema ifikapo Jumatatu ya kuanzia tarehe 20 Machi mwaka huu mbegu hizo ziwe zimesambazwa kwa wakulima wenye mahitaji au Halmashauri ilipe fedha za mbegu hizo.
Hata hivyo RC amewataka Watumishi hasa Maafisa kilimo kutokaa ofisini badala yake wakawasaidie wakulima na kuhakikisha wanapata mbegu hizo.
Katibu Tawala Msaidi Selestian Choaji ameeleza kwamba zaidi ya Tani 100 za mbegu za alizeti zenye ruzuku hazijawafikia wakulima na kwamba zipo mikononi mwa watendaji wakata na Vijiji.
Serikali ya Mkoa wa Singida kupitia vikao vyake iliomba kupatiwa mbegu za alizeti zenye ruzuku ambazo wakulima wangekopeshwa halafu wangelipa wakati wa mavuno.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.