Katika kipindi cha Mwezi Julai hadi Oktoba 2023, Mkoa umepokea fedha kwa ajili ya kutekeleza shughuli za maendeleo kiasi cha Shilingi 34,625,861,519.81 ambapo ngazi ya Halmashauri ni Shilingi 33,080,647,269.81 na ngazi ya Mkoa ni Shilingi 1,545,214,250. Ikiwa fedha za miradi ya ujenzi ni shilingi 545,000,000/=, Uratibu mfuko wa pamoja wa afya ngazi ya Mkoa shilingi 48,438,250/=, usimamizi na uratibu wa shughuli za mitihani shiling 33,5888,000/= na Usimamizi na Ufuatiliaji shilingi 280,000,000/=.
Fedha zilizopokelewa ni kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya elimu, afya, utawala, ununuzi wa vifaa katika vituo vipya vya kutolea huduma za Afya, uboreshaji wa huduma za afya kupitia mfuko wa Pamoja wa Afya (HSBF) na ugharamiaji wa Mpango wa Elimu Bila Malipo na mitihani.
Pamoja na taarifa hii kuna mchanganuo wa miradi iliyopokea fedha kwa kipindi cha Mwezi Julai - Oktoba, 2023.
Nawasilisha.
*BONYEZA HAPA* Fedha za Maendeleo kipindi Julai - Oktoba 2023 Mkoa Singida.xls
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.