Lishe ni moja ya vitengo vinavyotoa huduma chini ya idara ya afya Mkoani Singida. Lengo kuu la kitengo ni kuhakikisha kuwa matatizo makuu ya lishe yanatatuliwa ili kupata jamii yenye lishe na afya bora.
Kutokana na utafiti wa Afya ya mama na Mtoto (Tanzania Demographic survey) wa 2015, ilitoa takwimu ya viashiria mbalimbali za lishe. Kwa Mkoa wa Singida Matokeo ya utafiti huo ulionesha kuwa 29% ya watoto chini ya miaka mitano wana udumavu, 4.7% wana ukondefu na 11.7% wana uzito wa chini ukilinganisha na umri wao na 36% wana upungufu wa damu.
Kwa upande wa wanawake waliokatika umri wa kuzaa(15-49 miaka),asilimia 8.8% wana ukondefu, 16% wana uzito uliozidi, 6% wana uzito mkubwa sana na 26% wana upungufu wa damu. Pia ilionekana 64% ya kaya katika mkoa wa Singida wanatumia chumvi isiyo na madini joto.
Huduma za lishe zinazotolewa katika hospitali ya Mkoa ni pamoja na;-
Bonyeza hapa ili kupata taarifa zaidi kuhusu Lishe
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.