SEHEMU YA SERIKALI ZA MITAA
Sehemu ya menejimenti ya huduma za Serikali za Mitaa ni miongoni mwa sehemu/kitengo katika muundo wa uongozi katika Sekretarieti ya Mkoa ambayo kazi yake kubwa ni kutoa ushauri wa kitaalam, kusimamia utekelezaji wa majukumu mbalimbali katika Mamlaka za Serikali za mitaa katika nyaja za utawala bora, usimamizi wa makusanyo ya mapato ya ndani na matumizi ya fedha za umma, utekelezaji wa sheria za nchi na sheria ndogo za Halmashauri, masuala ya kiutumishi na uandaaji wa Mipango na Bajeti.
Sehemu ya Menejimenti ya Huduma za Serikali za mitaa inaongozwa na Bw. Evodius R. Katare - Katibu Tawala Msaidizi anayehusika na usimamizi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika Mkoa wa Singida
PICHA YA KATIBU TAWALA MSAIDIZI
MAENEO YA USIMAMIZI
Sehemu ya Serikali za Mitaa inazisimamia Halmashauri saba za Mkoa wa Singida ambazo ni Halmashauri za Wilaya ya Ikungi, Iramba, Itigi, Manyoni, Mkalama, Singida na Halmashauri ya Manispaa ya Singida. Halmashauri hizi zipo katika Wilaya tano (5) za Mkoa wa Singida ambazo ni
Halmashauri za Wilaya zinaongozwa na Wenyeviti wa Halmashauri na Halmashauri ya Manispaa inaongozwa na Mstahiki Meya. Watendaji wakuu wa Halmashauri za Wilaya ni Wakurugenzi watendaji wa Halmashauri na mtendaji mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ni Mkurugenzi wa Manispaa. Halmashauri hizo zina Tarafa, Kata, Vijiji na vitongozi kama ifuatavyo:
MAJUKUMU YA SEHEMU YA MENEJIMENTI YA HUDUMA ZA SERIKALI ZA MITAA
Majukumu ya Sehemu ya Menejimenti ya Huduma za Serikali za Mitaa ni pamoja na:-
MAFANIKIO YA SEHEMU YA SERIKALI ZA MITAA KWA MWAKA 2021/2022
Idadi ya Majimbo ya Uchaguzi na Kata zake
Na
|
Wilaya
|
Jimbo la Uchaguzi
|
Halmashauri
|
Idadi ya Tarafa
|
Idadi ya Kata
|
1.
|
Singida
|
Singida Kaskazini
|
Singida DC
|
03 |
21 |
Singida Mjini
|
Singida MC
|
02 |
18 |
||
2.
|
Manyoni
|
Manyoni Mashariki
|
Manyoni DC
|
04 |
19 |
Manyoni Magharibi
|
Itigi DC
|
01 |
13 |
||
3.
|
Iramba
|
Iramba Magharibi
|
Iramba DC
|
04 |
20 |
4.
|
Mkalama
|
Iramba Mashariki
|
Mkalama DC
|
03 |
17 |
5.
|
Ikungi
|
Singida Mashariki
|
Ikungi DC |
02 |
13 |
Singida Magharibi
|
02 |
15 |
|||
|
Jumla
|
|
|
21 |
136 |
NB: Majimbo yote nane (8) yanaongozwa na CCM. Pia kuna wabunge 2 wa viti maalum CCM
Idadi ya Waheshimiwa Madiwani wa Kata na Viti maalum
Na
|
Halmashauri
|
Idadi ya Madiwani wa Kata
|
Idadi ya Madiwani wa Viti maalum
|
Jumla
|
1.
|
Singida DC
|
21 |
7 |
28 |
2.
|
Manynoni DC
|
19 |
7 |
26 |
3.
|
Iramba DC
|
20 |
7 |
27 |
4.
|
Mkalama DC
|
17 |
6 |
23 |
5.
|
Ikungi DC
|
28 |
10 |
38 |
6.
|
Itigi DC
|
13 |
5 |
18 |
7.
|
Singida MC
|
18 |
6 |
24 |
|
Jumla
|
136 |
48 |
184 |
NB: Madiwani wa Kata wanawake wapo 04 kati ya 136 sawa na asilimia 2.9 ya madiwani wa Kata. Kata hizo ni Sepuka (Ikungi), Shelui (Iramba), Itigi Majengo (Itigi), na Majengo (Singida Manispaa).
Madiwani wa Kata CCM-135 na CHADEMA 01.
Katika eneo hili Halmashauri zote saba za Mkoa wa Singida zilipata HATI INAYORIDHISHA katika ukaguzi uliofanywa kwa mwaka 2020/2021 na mdhibiti na mkaguzi mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG)
Halmashauri za Mkoa wa Singida zimepewa mamlaka ya kukusanya mapato ya ndani ya Halmashauri kutoka kwenye vyanzo mbalimbali vilivyopo katika Halmashauri hizo, Chanzo kikubwa cha mapato katika Halmashauri za Mkoa wa Singida ni chanzo cha ushuru wa mazao ambapo asilimia 80 ya wakazi wa Mkoa wa Singida wanajishughulisha na kilimo. Kwa kipindi cha Julai 2021 hadi Juni, 2022 jumla ya sh 13,641,188,076.13 zimekusanywa kati ya lengo la kukusanya sh. 16,881,647,081.00 sawa na utekelezaji wa asilimia 81. Mchanganuo ufuatao unaonesha utekelezaji kwa kila Halmashauri:
Ushirikishwaji wa wananchi katika ushiriki na utekelezaji wa uandaaji wa Bajeti kwa ngazi za vijiji na kata pamoja na utekelezaji wa Miradi ya maendeleo unafanyika kwa kutumia Mpango wa Fursa na Vikwazo kwa maendeleo ulioboreshwa (Improved O&OD) ambapo kwa Mkoa wa Singida mpango ulianza kutekelezwa rasmi mwezi Julai, 2017 kwa kutoa mafunzo mbalimbali kwa viongozi wa Mkoa na Halmashauri hasa waheshimiwa Madiwani, wakuu wa idara na vitengo wa Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na Maafisa Ugani wa Kata (Maafisa Maendeleo ya jamii, maafisa mifugo na maafisa kilimo) ambapo baada ya mafunzo hayo wananchi wa Mkoa wa Singida walielimishwa pia kuhusu umuhimu wa ushiriki wao katika kupanga na kutekeleza miradi ya maendeleo katika maeneo yao ili kuweza kutatua kwa urahisi changamoto zinazowakabili, kuwa na umiliki na uendelezaji wa Miradi hiyo.
Mafanikio yaliyopatikana katika ushirikishwaji wa jamii ni kama ifuatavyo:
Ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi moja katika shule shikizi ya kijiji cha Ntonge, Halmashauri ya Wilaya ya Singida.
Picha kutoka kushoto inaonyesha ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa na ofisi unaoendelea katika shule ya Msingi Makutupora, Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni na picha inayofuata inaonyesha Katibu Tawala wa Mkoa Singida akipokea taarifa ya utekelezaji wa mradi huo kutoka kwa viongozi wa Kijiji cha Makutupora.
MAJUKUMU YA SEHEMU YA MENEJIMENTI YA SERIKALI ZA MITAA
Majukumu ya Sehemu ya Menejimenti ya Huduma za Serikali za Mitaa ni pamoja na:-
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.