Seksheni hii ina lengo la kutoa huduma za kitaalamu zinazohitajika kwa Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuendeleza Miundombinu na inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi ambaye anawajibika kwa Katibu Tawala wa Mkoa.
Majukumu ya Seksheni ya Miundombinu:
•Kuratibu utekelezaji wa Sera, Sheria, Kanuni na Viwango katika nyanja za Barabara, Majengo, Nishati, Upimaji, Ardhi na Mipangomiji
•Kuzijengea uwezo Mamlaka za Serikali za Mitaa katika nyanja za Barabara, Majengo, Nishati, Upimaji, Ardhi na Mipangomiji
•Kuwasiliana/kuwa daraja kuunganisha baina ya Mamlaka zinazohusika kwenye Serikali Kuu na Mamlaka za Serikali za Mitaa juu ya masuala ya Ujenzi
•Kushauri juu ya Masuala ya barabara, Nishati, Ujenzi, Viwanja na uboreshaji mifumo
•Kusimamia na kushauri juu ya kazi za Ujenzi zinazotekelezwa ndani ya Mkoa
•Kuzisaidia Mamlaka za Serikali za Mitaa kutwaa ardhi kwa ajili ya matumizi ya Serikali Kuu
•Kuandaa ramani kwa ajili ya mipangomiji
•Kumshauri Katibu Tawala wa Mkoa juu ya Tathimini ya Athari za Kimazingira
•Kuzishauri Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kuendeleza maeneo ya wanyamaporI
Seksheni hii inaongozwa na Katibu Tawala Msaidizi anayeshughulika na Miundombinu
UJENZI WA DARAJA LA SIBITI (mita 82) - TANROADS
Daraja la Sibiti liko mpakani mwa Mikoa ya Singida na Simiyu, katika mto Sibiti kwenye barabara ya Mkoa ya Ulemo – Gumanga – Sibiti (km 76). Mradi huu ulihusisha ujenzi wa daraja lenye urefu wa meta 82 na barabara za maingilio ya changarawe (approach roads) zenye urefu wa km 25 kutokea Chemchem hadi Kijiji cha Bukundi Mkoa wa Simiyu. Mradi uligharamiwa na Serikali ya Tanzania kwa asilimia 100. Gharama ya mradi ni Shilingi 28,511,511,000.00. Kazi za ujenzi ilikamilika tangu mwezi Machi, 2019. Katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali ilitenga jumla ya Shilingi 2,500.000milioni kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara za maingilio ya daraja la mto Sibiti km 25 kwa kiwango cha lami, ikiwa upande wa Bukundi km 5 na upande wa Singida km 20.
DARAJA LA MSINGI -TANROADS
kazi ya kumwaga lami nyepezi katika barabara za maingilio ya daraja. Daraja la msingi lina urefu mita 75. Barabara za maingilio zina urefu wa kilomita 1 ambayo ni sawa na mita 500 kila upande wa kuingia darajani. Daraja hili limegharimu shilingi za kitanzania 9,002,573,250.00 kazi ipo hatua za mwisho.
Daraja hili linaunganisha barabra itokayo Dar es salaam kwenda Mwanza na Barabara itokayo Iguguno kwenda Nduguti - Gumanga - Ibaga – Bukundi hadi Simiyu.
DARAJA LA MAWE MSINGI - TARURA
Daraja hili lilijengwa mwaka 2018, liligharimu shilingi za kitanzania 250,000,000.00 linaunganisha Tarafa ya Nduguti na Tarafa ya Kinampanda, pia linawezesha njia ya mchepuko kutoka Nduguti kupitia Isinshi na baadae kufika kijiji cha Msingi, barabara hii hutumika pale ambapo mtu anayetoka Kinampanda hataki kufika Gumanga. Mradi huu umetekelezwa na TARURA kwa gharama ya shilingi za kitanzania 222,988,954.00. Daraja lina urefu wa mita 45, upana mita 8 na midomo 4.
DARAJA LA MAWE ENDASIKU - TARURA
Daraja hili ni mradi unaotekelezwa na TARURA. Baada ya matokeo mazuri ya daraja la mawe Msingi TARURA Singida imeongeza ujenzi wa vivuko vya mawe katika Mkoa wa Singida. Kwakuwa Mkoa wa Singida umebarikiwa kuwa na mawe mengi. Daraja la Endasiku lina urefu mita 30, upana mita 7 na lina midomo 4, limegharimu shilingi za kitanzania 156,601,000.00 linaunganisha kijiji cha Endasiku, Nyahaa, Matala na Mwengeza.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.