UTANGULIZI:
Wilaya ya Ikungi ni miongoni mwa Wilaya tano (5) zilizopo Mkoa wa Singida. Wilaya hii iliundwa mnamo tarehe 02 Machi, 2012 kupitia Tangazo katika Gazeti la Serikali GN. Na. 73.
ENEO LA GEOGRAPHIA:
Wilaya ya Ikungi ina ukubwa wa Km2 8860 Wilaya ya Ikungi ipo kati ya Nyuzi 40 na 60 Latitudo Kusini mwa Ikweta, Nyuzi 340 na 350 ya Ikungi kupata mvua wastani wa mm 600-700 kwa mwaka na joto kati ya 150c - 300c.
Wilaya ya Ikungi inapakana na Wilaya ya Uyui (Mkoa wa Tabaora) upande wa Magharibi, Wilaya ya Singida Upande wa Kaskazini Wilaya ya Iramba upande wa Kaskazini Magharibi, Wilaya ya Manyoni upande wa Kusini na Wilaya ya Chemba upande wa Kusini Mashariki.
SHUGHULI ZA KIUCHUMI:
Wananchi wa Wilaya ya Ikungi hujishughulisha na shughuli za Kilimo, Ufugaji, uchimbaji wa Madini hasa dhahabu na Almasi, Biashara pamoja na Uvuvi.
UTAWALA:
Wilaya ya Ikungi ina Halmashauri moja ya Wilaya, Majimbo Mawili ya Uchaguzi, Jimbo la Singida Mashariki na Jimbo la Singida Magharibi, Tarafa 4 za Mungaa, Ikungi, Ihanja na Sepuka pamoja na Kata 28, Vijiji 101 na Vitongoji 5389.
UONGOZI:
Wilaya ya Ikungi inaongozwa na Mkuu wa Wilaya akisaidiwa na Katibu Tawala wa Wilaya. Mkuu wa Wilaya wa sasa anaitwa Mhe. Jerry C. Muro na Katibu Tawala anaitwa Bi. Winfrida E. Funto.
ORODHA YA WAKUU WA WILAYA WALIOONGOZA IKUNGI:
ORODHA YA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA WALIOFANYA KAZI IKUNGI
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.