• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

Baraza la Wafanyakazi lazinduliwa rasmi, Watumishi waaswa kuongeza tija katika bajeti ijayo.

Posted on: March 9th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba amewataka Watumishi wa Mkoa huo kufanya kazi kwa bidii ili kupatikana tija itakayo saidia kuongeza mapato ambayo yataboresha maslahi ya Watumishi.

Kauli hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la Wafanyakazi lililofanyika Machi 9, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi hiyo ambapo alisistiza uwepo wa mahusiano mazuri baina ya watumishi ili kuongeza tija.

"Pia nipende kusisitizia kuwa bila tija Serikali haiwezi kupata mapato ambayo yataiwezesha kuboresha maslahi ya watumishi" alisema Serukamba

Aidha ameagiza Baraza hilo  kutekeleza majukumu yake kuhusu taratibu zinazoweza kuchukuliwa ili kuleta ufanisi katika mifumo ya kutoa huduma kwa wananchi na kushauri mabadiliko ya kanuni za kudumu katika utumishi wa umma namna bora ya kuboresha mazingira. Serukama aliagiza wajumbe wa Baraza hilo kuhakikisha wanapitia rasimu ya bajeti kwa undani na kushauri kama kuna maeneo hayo yalisahaulika kabla havijafikishwa bungeni.

Hata hivyo RC Serukamba ameagiza Halmashauri zote Mkoani hapo ambazo mabaraza yake ya wafanyakazi yalimaliza muda wake kuhakikisha wanachagua mengine ili yaweze kuendelea kutetea maslahi ya watumishi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Baraza hilo ambaye pia ni Katibu Tawala Mkoa Mwl. Dorothy Mwaluko amewaasa watumishi kutumia weledi katika kutekeleza majukumu ili kuleta tija iliyo kusudiwa huku akikumbusha kufuata mila na desturi za utumishi ili kufikia malengo.

"Utumishi una mila na desturi zake na mtumishi atapata tabu endapo atashindwa kuzifuata, tuishi maisha ya utumishi wa umma" Mwaluko

Aidha amehimiza watumishi kuwa wavumilivu na upendo katika kufanya kazi huku akibainisha kwamba hakuna mwenyekazi zake binafsi katika Mkoa hivyo watumishi wajifunze kushirikiana katika kutumia rasilimali zilizopo zikiwemo magari.



Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.