• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

MALIGHAFI ZAIDI ZAHITAJIKA ILI KUINUA VIWANDA MKOANI SINGIDA

Posted on: January 22nd, 2026

Mkoa wa Singida umetajwa kuwa na fursa kubwa ya kukuza uchumi wa viwanda, lakini bado unakabiliwa na changamoto ya uhaba wa malighafi unaosababisha baadhi ya viwanda kusimamisha uzalishaji. Kauli hiyo imetolewa na Brigedia Jenerali Charles  Ndiege wakati wa ziara ya mafunzo kwa vitendo ya washiriki wa kozi ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi waliotembelea viwanda mbalimbali mkoani humo.

Akizungumza baada ya kutembelea viwanda vya kuchakata alizeti na pamba, Brigedia Jenerali Ndiege amesema changamoto kubwa iliyojitokeza ni viwanda kushindwa kufanya kazi kwa msimu mzima kutokana na utegemezi wa malighafi zinazotokana na kilimo cha mvua. Amesema hali hiyo huathiri mnyororo mzima wa maendeleo ya kiuchumi, kuanzia wakulima hadi wafanyakazi wa viwandani.


Amefafanua kuwa viwanda vinaposimama, ajira hupungua na mapato ya wananchi hushuka, hali inayodhoofisha mchango wa sekta ya viwanda katika pato la taifa. Kwa mtazamo wake, uzalishaji wa viwanda hauwezi kuwa endelevu bila sera madhubuti zitakazohakikisha upatikanaji wa malighafi kwa uhakika na kwa wingi.

Brigedia Jenerali Ndiege amesisitiza kuwa kuongeza uzalishaji wa mazao ya viwandani ni ajenda ya kimkakati kwa taifa, akibainisha kuwa masuala ya chakula na viwanda yanagusa moja kwa moja usalama wa taifa. Ameshauri kuimarishwa kwa kilimo cha tija, matumizi ya teknolojia na ushirikiano wa karibu kati ya serikali, wakulima na wawekezaji wa viwanda.

Kwa upande wa washiriki wa kozi hiyo, Hawa Adam kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema ziara hiyo imewapa uelewa wa kina kuhusu mchango wa viwanda vya Singida katika kukuza uchumi wa taifa. Amesema viwanda hivyo vinatoa soko la uhakika kwa wakulima na hivyo kuboresha maisha yao kupitia kipato na upatikanaji wa huduma za kijamii.

Ameongeza kuwa changamoto ya uzalishaji mdogo inaweza kutatuliwa kwa kutoa elimu zaidi kwa wakulima juu ya mbinu bora za kilimo ili kuongeza mavuno ya mazao yanayotumika kama malighafi viwandani, hatua itakayosaidia viwanda kufanya kazi kwa ufanisi zaidi.

Aidha, Wawakilishi wa viwanda vya Biosustain Tanzania Limited na Mount Meru Millers Limited wameeleza kuwa uzalishaji mdogo wa pamba na alizeti bado ni changamoto kubwa, wakisisitiza umuhimu wa kuendelea kuhamasisha wakulima kuongeza uzalishaji. Wamesema kupitia elimu, motisha na ushirikiano na serikali, uzalishaji unaweza kuongezeka na kuwezesha viwanda kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi.

Ziara ya washiriki wa kozi ya Chuo cha Taifa cha Ulinzi mkoani Singida ni sehemu ya mafunzo kwa vitendo yanayolenga kuoanisha nadharia za darasani na utekelezaji wa sera, mipango na mikakati ya serikali katika mazingira halisi. Kupitia ziara hiyo, washiriki wanapata fursa ya kutathmini maendeleo ya viwanda, kilimo na uchumi kwa ujumla, pamoja na kubaini changamoto na fursa zilizopo kwa maendeleo endelevu ya taifa.

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • MALIGHAFI ZAIDI ZAHITAJIKA ILI KUINUA VIWANDA MKOANI SINGIDA

    January 22, 2026
  • MADIWANI WATAKIWA KUSIMAMIA MIRADI,MAPATO NA NIDHAMU KWA WATUMISHI

    January 15, 2026
  • CHANGAMOTO ZA WAFUGAJI NA WAVUVI SINGIDA ZAANZA KUPATIWA UFUMBUZI

    January 10, 2026
  • WANANCHI WAGUSWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA KISHERIA MKOANI SINGIDA

    January 09, 2026
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.