Katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi CCM Ndg. Daniel Chongolo amekemea Baadhi ya Wazazi na Walezi nchini ambao wameshindwa kusimamia na kuwaongoza Vijana wao kuzingatia Suala la Maadili hususani Tabia zao na Mavazi wanayovaa.
Kauli hiyo ya Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ameitoa Singida Vijijini katika Kijiji cha Mtinko, baada ya hoja ya maadili kuibuliwa na Mzee Emmanuel Mgoya aliyehudhuria kikao cha Shina namba 2 ambacho Katibu Mkuu alihudhuria.
Akizungumza mbele ya Katibu mkuu wa CCM, Mzee Mngoya ameeleza kuhuzunishwa na Kuporomoka kwa maadili ya Vijana wa kiume na Watoto wa Kike na
"Ndugu Katibu Mkuu wa CCM Sasa hivi hali imekuwa mbaya mbaya mno kwa Wanawake wanavaa Uchi na Hawana Mavazi ya Staha, Jambo hili linanikera mno, ninakuomba Umwambie Rais Mama Samia Suluhu Hassan kwamba huku mtaani Baadhi ya Wanawake wanatembea Uchi" amesema Mzee Mngoya.
Akijibu hoja na Maelezo ya Mwananchi huyo wa Kijiji cha Mtinko, Katibu mkuu Chongolo amesema Tanzania imejengwa kwa misingi mizuri ya Maadili, ambapo Wazazi na Walezi wanapaswa kubadilika kwa Kuhakikisha Wanasimamia Maadili ya Vijana wao ili kuenenda vyema na Maadili ya Kitanzania.
"Siku hizi Vijana wetu hasa wa kike akitoka nyumbani anavaa vizuri kajifunga na kanga, kumbe akitoka ile kanga anaitia kwenye mkoba halafu anabaki na mavazi ya ajabu, Hii ni Aibu hata ukikutana nae mtaani, lazima tubadilike lazima tuenzi na kulinda Utamaduni wa Mtanzania leo, kesho na Keshokutwa" amesema Katibu Mkuu Ndg. Chongolo.
Katibu mkuu wa CCM Daniel Chongolo anaendelea na Ziara yake mkoani Singida akiambatana na Katibu wa NEC itikadi na Uenezi wa Chama Ndg. Sophia Mjema pamoja na Katibu wa Halmashauri kuu ya CCM Taifa Oganaizesheni Ndg. Issa Haji Gavu.
Mwisho.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.