Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida Daktari Fatuma Mganga ametoa maagizo ya kuhakikisha Halmashauri zote zinafunga mashine za kuongeza virutubishi vya lishe ili kuhakikisha wananchi pamoja na wanafunzi mashuleni wanapata chakula chenye virutubisho muhimu kwa ajili ya kuimarisha afya zao.
Ameyasema hayo leo Mei 12,2025 katika kikao cha Kamati ya lishe cha Mkoa kilichofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida kikihusisha wadau mbalimbali wakiwemo wajumbe wa Kamati hiyo,wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa,na wadau kutoka Taasisi mbali mbali.Sambamba na hilo amepongeza matumizi mazuri ya mfumo wa GoTHOMIS kwa ajili ya ukusanyaji mzuri wa taarifa mbalimbali za afya na kutoa maagizo ya kuhakikisha wananchi wanahamasishwa kujiunga na matumizi ya Bima ya Afya.
Katibu wa kikao hicho Dkt.Victorina Ludovick(Mganga Mkuu wa Mkoa)amewasilisha utekelezaji wa maazimio mbali mbali katika kikao ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya mashine za kuongeza virutubishi kwenye unga wa mahindi,kuhakikisha wakinamama wajawazito wote wanapimwa wingi wa damu kwa asilimia zaidi ya 95,kufanya uchambuz iwa kina kwenye utoaji wa huduma ya Vitamini A kwa wakina mama waliojifungua na utoaji wa dawa za minyoo kwa watoto chini ya miaka mitano na kuandaa taarifa inayoonyesha vituo vyenye changamoto katika utoaji wa huduma hizo.
Kadhalika amesema kuwa kila shule inapaswa kuainisha kiasi cha chakula kilichovunwa ukilinganisha na kiasi cha mazao kilicholimwa kwenye shule husika.
Kwa upande wa matumizi ya teknolojia katika utaoaji wa huduma,Dkt.Victorina amesema kuwa hali ya matumizi ya mfumo wa Serikali wa Taarifa za uendeshaji wa huduma za Afya,(GoTHOMIS) katika vituo vya afya ambapo matumizi yake yamefikia asilimia 95.Pia utekelezaji wa agizo la ufungaji wa mfumo mpya wa Centralized GoTHOMIS ambapo vituo 258 kati ya 272 vimetekeleza.
Akiwasilisha Viashiria vya upatikanaji wa lishe Mkoani Singida ,Afisa lishe mkoa Bi.Teda Sinde amesema lishe hupimwa kwa vigezo mbali mbali ikiwemo idadi ya wakina mama waliojifungua na kipata matone ya Vitamin A,idadi ya watoto walionyonya maziwa ya mama ndani ua lisaa limoja baada ya kuzaliwa,idadi ya wajawazito waliohudhuria kliniki ya wenye mimba chini ya wiki 12,hali ya utoaji wa vyakula vilivyoongezea virutubishi katika shule za msingi,hali ya mavuno katika mashamba ya Shule za Msingi ikiwemo karanga,alizeti,maharage,kunde,mahindi,mtama na mpunga.
Akifunga kikao hicho kwa niaba ya Mwenyekiti wa kikao Bw.Romwald Mwendi amesema kuwa ni vema kufatilia suala la takwimu za afya ili kuhakikisha taarifa zinazowasilishwa zinakua na usahihi na kurahisisha utafutaji wa suluhu pale tatizo linapoonekana na kurudisha nyuma maendeleo ya upatikanaji wa lishe kwa wananchi.Pia amesema kuwa Serikali imetoa kiasi cha Shilingi Bilioni 2.7 kwa ajili ya kumalizia miradi ya ujenzi wa majengo ya afya na elimu ambayo yalikua hayajakamilika ikiwemo madarasa,zahanati,mabweni nakadhalika kwa lengo la kuhakikisha kuwa huduma zinawafikia wananchi katika mazingira mazuri.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.