Katibu Tawala Mkoa wa Singida Mwl. Dorothy Mwaluko ameongoza mdahalo katikaShule ya Sekondari ya Wasichana Tumaini iliyopo Wilaya ya Iramba Tarehe 05 Machi, 2023.
Moja ya Mada iliyojadiliwa ni Mila na Desturi za Msichana wa Kitanzania katika Ulimwengu wa Kidigitali.
"Mila na Desturi zipi zinapaswa kuenziwa na msichana wa kitanzania na zipi zinapaswa kuachwa na msichana wa kitanzania".
Washiriki ambao ni Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Tumaini wamesema mila na Desturi zinazopaswa kuachwa kwa msichana wa kitanzania ni pamoja na kuozesha watoto wa kike wakiwa na umri mdogo, ukeketaji kwa watoto wa kike, kutokuwapeleka shule watoto wa kike na mengineyo.
Mila na Desturi zinazopaswa kuenziwa kwa watoto wa kike ni pamoja na kutokushiriki tendo la ngono kwa msichana akiwa na umri mdogo, kushiriki shughuli za maendeleo, kusoma kwa bidii na kupata elimu kwa usawa.
"Watoto wa kike mnapaswa kuwa wasafi wakati wote hasa nyakati za hedhi na ioneni kama ni hali ya kawaida ili muendelee na masomo mnapokua katika hali hiyo" Mwl. Dorothy Mwaluko
Kuweni wajasiri kwa kuwa na misimamo na kuhakikisha mnatimiza ndoto zenu, pamoja na changamoto mnazopitia lakini hakikisheni mnasoma kwa bidii na maarifa ili kutimiza ndoto zenu. Amesisitiza Mwl Mwaluko
Aidha amewataka Watoto wa kike kutumia utandawazi kwa kujifunza mila na desturi nzuri za Kitanzania ili muendelee kuzidumisha kwenye maisha yao ya kila siku na sio kutumia utandawazi vibaya.
Mwaka huu Singida inafikisha miaka 60 hivyo tutakua na maadhimisho hayo kimkoa yatakayo fanyika Oktoba, hivyo ametumia fulsa hiyo kuwaomba wajiandae kwa midahalo, maonesho ya mavazi na burudani zingine ili siku hiyo iwe yenye shamrashara furaha na nderemo.
Naye Katibu wa Chama cha Walimu Mkoa wa Singida Mwl. Digna Nyaki amesema wataendelea kuhakikisha malezi ya watoto wao yanakua mazuri na kuwalinda watoto wa kike ili kujenga Taifa la bora lenye amani uzalenda na utulivu.
Hata hivyo Mwl. Nyaki amesema watahakikisha watoto wa kike wanapata elimu kwa usawa bila kubaguliwa maana watoto wa kike wana haki sawa na watoto wa kiume.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.