Serikali imekabidhi magari yenye thamani ya Sh.Bilioni 1.009 kwa wakuu wa Wilaya nne za Mkoa wa Singida ili kurahisisha utendaji kazi katika kuwahudumia wananchi.Wakuu wa wikaya waliopata magari hayo ni Ikungi,Iramba,Singida na wilaya ya Manyoni.
Tukio hilo limefanyika katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Singida leo Mei 19,2025 likishuhudiwa na Katibu Tawala wa Mkoa,Wakuu wa Wilaya,Wakuu wa Sehemu na vitengo na watumishi wengine.
Mkuu wa Mkoa wa Singida,Mhe.Halima Dendego, amekabidhi magari hayo kwa Wakuu wa Wilaya za Ikungi, Iramba, Manyoni na Singida na kufanya idadi ya magari yaliyotolewa kwa mkoa huu kwa kipindi cha miaka miwili kufikia yenye thamani ya Sh.bilioni 2.695.
"Wakati tunasubiri magari haya wapo wakuu wa idara na vitengo tuliwanyima fursa ya kuwa na vyombo vya usafiri ili kuwawezesha ma-DC kufanya kazi leo tunarudisha nguvu kwenye sekretarieti ya Mkoa wa Singida na yenyewe iungane na Sekretarieti ya Mkoa, Katibu Tawala Mkoa na Mkuu wa Mkoa katika kuwafikia wananchi," amesema Mhe.Dendego.
Mhe.Dendego ametaka magari hayo kutunzwa vizuri sambamba na kuzingatia ratiba ya matengenezo (service) kama taratibu zilivyowekwa ili yaweze kudumu muda mrefu kwani Serikali imetumia fedha nyingi katika kuyanunua kwa lengo la kuhakikisha yanafanya kazi za maendeleo kwa jamii zilizokusudiwa.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Singida,Dkt.Fatuma Mganga, amesema kuwa katika mwaka wa fedha wa mwaka jana ,Mkoa huu ulikuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa magari kwa ajili ya viongozi wandamizi wa serikali.
"Tunamshukru sana Rais Dk.Samia Suluhu Hassan sasa hivi tumepata gari ya Mkuu wa Mkoa yenye thamani ya Sh.milioni 470, gari ya Katibu Tawala Mkoa ya Sh.milioni 393 na jumla magari yote tuliyopata kama mkoa yana thamani ya jumla ya Sh. bilioni 2.695," amesema.
Mkuu wa Wilaya ya Ikungi, Thomas Apson,akizungumza kwa niaba ya wakuu wa wilaya alisema magari waliyopewa yatawasaidia utendaji kazi na kuwafikia wananchi kwa haraka kuwahudumia.
"Kwa kweli Tunamshukru sana Mheshimiwa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa magari hayo hakika ni gari za kazi kweli ambazo zinatuwezesha kufika mahali popote walipo wananchi na kuwahudumia ipasavyo,"alisema Apson.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.