Halmashauri za Mkoa wa Singida zimetakiwa kutenga fedha katika mipango na bajeti zake kwa ajili ya gharama za usafiri wa dharura kwa Mama wajawazito na watoto wachanga.
Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba leo Novemba 22, 2022 wakati akifungua kikao cha Uzinduzi wa Mpango wa Usafirishaji wa dharura kwa akina Mama wajawazito, waliojifungua na watoto wachanga (M-Mama) kwa Mkoa wa Singida.
Rc Serukamba ameelekeza kwamba mfumo huo utakuwa ni msaada mkubwa kwa wananchi wa Singida kwakuwa utasaidia kupunguza vifo vya Mama wajawazito, wanaojifungua na watoto kwa kuweza kufikishwa Hospitali au vituo vya afya kwa wakati.
Amesema mpango wa huduma hiyo utaboresha zoezi la rufaa kati ya vituo vya kutolea huduma za Afya, hasa upatikanaji wa usafiri wa dharura kutoka kituo kimoja hadi kituo kinachoweza kutoa huduma ya viwango vya juu ambapo ameeleza kwamba utasaidia kupunguza changamoto ya upungufu kusubiria foleni ya magari ya wagonjwa.
“Kama tunavyofahamu huduma za Afya ya Mama na Mtoto hutolewa bila malipo, kwa hiyo hatua mbalimbali za kuhakikisha huduma bora zinapatikana katika Mkoa wetu wa Singida, ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya vituo vya kutolea huduma za Afya vinavyotoa huduma kamili za dharura na Upasuaji kutoka vituo vya huduma sita (6) mwaka 2020 hadi saba (7) mwaka 2022” amesema Serukamba
Mkuu wa Mkoa wa Singida Peter Serukamba akisoma hotuba yake mbele ya washiriki wa zoezi la uzinduzi rasmi wa Mfumo wa M-Mama uliyofanyika kimkoa katika ukumbi wa mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Kwa upande wake Mratibu wa afya ya uzazi na mtoto Mkoa wa Singida Christoweru Barnaba wakati akitoa wasilisho lake amesema mradi huo utasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza vifo vya mama na mtoto.
Aidha ameleeza kwamba uwepo wa changamoto ya Upungufu mkubwa wa magari (Ambulance) za kubebea wazazi na wagonjwa wanaohitaji rufaa hasa Halmashauri ya Itigi, Mkalama, Singida, Ikungi kwa uwepo wa mradi huo utasaida kwa kuwa magari binafsi yatasajiliwa kwa ajili ya kupeleka wagonjwa.
Akimalizia wasilisho lake Christoweru ametoa wito kwa mama wajawazito kuacha tabia ya kujifungulia nyumbani au njiani na badala yake wahakikishe wanafika hospitalini ili waweze kukutana na wataalamu.
Mratibu wa Afya ya uzazi na mtoto Mkoa wa Singida Christoweru Barnaba, akiwasilisha mada wakati wa uzinduzi huo.
Aidha Mkurungenzi wa mfumo wa M-Mama Dolorosa Duncan kutoka Kampuni ya Vodafone foundation amesema Serikali kwa kushirikiana na Vodacom inatekeleza mfumo wa rufaa na usafiri wa dharura – M-Mama ambao umefanyiwa majaribio katika Wilaya za mkoa wa Mwanza na Shinyanga na kuona unafanya kazi kwa ufasaha.
Hata hivyo Dolorosa ameendelea kueleza kwamba mfumo huo kwa sasa umeanza kutekelezwa katika mikoa ya Shinyanga Lindi Mororgoro Dodoma Tanga na sasa Singida na Manyara ambapo utaendelea kutekelezwa katika mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwani.
Mkurungenzi wa mfumo wa M-Mama Dolorosa Duncan,akiwasilishamadawakati wa uzinduzi huo
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.