Serikali imeupongeza Mkoa wa Singida kwa kujiandaa vizuri katika uonyeshaji wa bidhaa mbalimbali zinazozalishwa katika mkoa huo hali ambayo itasaidia kuwavuta wawekezaji kuja kuwekeza katika sekta mbalimbali mkoani humo.
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Kilimo David Silinde, mara baada ya kutembelea banda la mkoa wa Singida kwa ajili ya kujionea shughuli zinazofanywa na mkoa huo katika Maonesho ya Kimataifa ya Nane Nane yanayofanyika katika Viwanja vya Nzuguni mkoani Dodoma.
Naibu Waziri Silinde amewasisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kuona na kujifunza teknolojia mbalimbali za kisasa ambazo zitawasaidia kuimarisha na kuboresha uzalishaji katika maeneo yao.
‘Natoa rai kwa wananchi wote hasa wa mikoa ya Kanda kati jitokezeni kwa wingi katika Maonesho ya Nane nane mkapate elimu na kujifunza namna ya kulima kisasa kilimo ili kuongeza tija katika uzalishaji, Amesisitiza Silinde.
Wakati huo huo, Viongozi mbalimbali wameendelea kutembelea mabanda ya maonyesho yakiwemo ya mkoa wa Singida ambapo Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Philip Mangula, naye ametembelea mabanda ya mkoa wa Singida ili kujionesha shughuli mbalimbali zinazofanywa na mkoa huo hasa katika maeneo ya Kilimo na Ufugaji.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.