• Wasiliana Nasi |
    • Malalamiko |
    • MMM |
    • Barua Pepe |
    • Blog |
Singida Regional Website

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Tovuti ya Mkoa wa Singida

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na dhima
    • Uongozi wa Mkoa
  • Utawala
    • Muundo
    • Idara
      • Utawala na Rasilimaliwatu
      • Mipango na Uratibu
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Miundombinu
      • Serikali za Mitaa
      • Afya
      • Elimu
      • Maji
    • Vitengo
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa Ndani
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Manunuzi na Ugavi
  • Wilaya
    • Ikungi
      • HISTORIA
    • Iramba
    • Manyoni
    • Mkalama
    • Singida
  • Halmashauri
    • H/W Ikungi
    • H/W Iramba
    • H/W Itigi
    • H/W Manyoni
    • H/W Mkalama
    • H/W Singida
    • H/M Singida
  • Fursa za Uwekezaji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Viwanda na Biashara
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Afya
      • Madaktari Bingwa
      • Huduma za Tiba
      • Huduma za Kinga
      • Ustawi wa Jamii
      • Afya ya Mazingira
      • Lishe
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba Wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti Mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo Mbalimbali
    • Investment Guide
  • Kituo Cha Habari
    • Picha
    • Video
    • Hotuba
    • Taarifa kwa Umma

RAS Singida atembelea Hospitali, vituo vya Afya

Posted on: November 8th, 2022

Katibu Tawala Mkoa wa Singida Mwl. Dorothy Mwaluko leo tarehe 8.11.2022 ametembelea Hospitali, vituo vya Afya na Zahanati vilivyopo Wilaya ya Singida vijijini na Mkalama ili kuona huduma za afya zinavyotolewa katika maeneo hayo.

 Akiwa katika ziara hiyo amekagua Watumishi na utendaji kazi wao vitendea kazi pamoja na usafi wa mazingira yanayozunguka maeneo hayo.

Dorothy akiwa katika Kituo cha Afya cha Kinyangiri kilichopo kata ya Kinyangiri Wilayani Mkalama  amewaagiza Waganga wafawidhi katika Hospitali, Zahanati na vituo vya Afya kusimamia huduma stahiki kwa wagonjwa, maadili ya kazi na utunzaji wa mazingira ya nje na ndani ya Hospitali ili kuboresha mandhari ya maeneo hayo.

"Nataka mpande miti katika maeneo yenu na pia nataka kuwe na utaratibu wa upangaji wa vitu Hospitalini (classification) kama ulivyo utaratibu" alisema Mwaluko

Katibu Tawala huyo akiwa Kinyangiri akamuagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Singida Daktari Victorina Ludovick kuhakikisha gari la wagonjwa aina ya landrova linafanyiwa matengenezo haraka ili liweze kutumika kwa ufanisi mkubwa.

Hata hivyo Mwaluko akaagiza kuanza kutumika majengo yote ambayo fedha za umma zimetumika zikiwemo nyumba za wafanyakazi wa sekta ya Afya kuanza kutumika haraka iwezekavyo.

Aidha akawataka viongozi wa Idara ya Afya Mkoani hapo kutafuta miradi mbalimbali ambayo itawasaidia kuendesha shughuli mbalimbali badala ya kutegemea fedha za Serikali.

Aidha ameiagiza timu ya  usimamizi na uendeshaji wa huduma za Afya ya Mkoa huo  (RHMT) kuwatembelea watumishi wa Afya mara kwa mara ili kuwafariji na kuona na kutatua changamoto zinazowakabili.

Naye Mganga mfawidhi wa Kituo cha Kinyangiri Daktari Anna Kimonga akamueleza Katibu Tawala Mkoa kwamba  Kituo hicho kinapokea  Wagonjwa kati ya 30 mpaka 50 na wanawake wanaojifungua ni kati ya 25 mpaka 30 kwa mwezi ambapo ameeleza kwamba ni muhimu kuwa na gari la Wagonjwa lenye uwezo wa kufanya kazi kulingana na mazingira.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mkalama  Daktari  Dorisila John amesema  upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika Wilaya hiyo unaridhisha huku akibainisha kwamba kwa mujibu wa muongozo bado Kkna uhitaji wa madaktari na wauguzi katika vituo vingi vya Afya na Zahanati Wilayani hapo.

Dorisila amesema katika Hospitali ya Wilaya ya Mkalama mpaka kufikia tarehe 16 Novemba, 2022 ufungaji wa vifaa vya X-Ray utakuwa umekamilika jambo ambalo wanategemea kwamba huduma za mashine hiyo zitaanza hivi karibuni.

Ziara hiyo ya Katibu Tawala Mkoa wa Singida aliambatana na timu ya usimamizi na uendeshaji wa huduma za Afya Mkoa (RHMT) ambapo walitembelea Zahanati ya Kanisa Katoliki Iguguno, Kituo cha Afya Kinyangiri, Hospitali ya Wilaya ya Mkalama, Hospitali ya rufaa ya Iambi, Hospitali ya Wilaya ya Singida na Kituo cha afya Ilongero.

Mwisho

Matangazo

  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2022_2023 SINGIDA RS July 01, 2022
  • MAJINA YA WALIOCHANGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA - 2023, MKOA WA SINGIDA December 14, 2022
  • TAARIFA YA MAPOKEZI YA FEDHA KWA KIPINDI CHA KUANZIA JULAI HADI OCTOBA, 2023 KWA AJILI YA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI ZA MAENDELEO November 01, 2023
  • GENERAL PROCUREMENT NOTICE FOR YEAR 2021/2022 SINGIDA RS - GPN 2021 - 2022 July 01, 2021
  • Angalia Zote

Habari Mpya

  • IKUNGI YAPEPERUSHA BENDERA KWA MIRADI YA KIMKAKATI.

    May 08, 2025
  • DKT.MGANGA ASISITIZA MADAKTARI BINGWA KUTOA HUDUMA BORA

    May 05, 2025
  • WATUMISHI NA WAAJIRI HODARI MKOANI SINGIDA WAPOKEA TUZO

    May 02, 2025
  • KUELEKEA MEIMOSI,RC DENDEGO ATANGAZA FURSA ZA UWEKEZAJI

    April 25, 2025
  • Angalia Zote

Video

Mkoa wa Singida waja na Mikakati ya Kuboresha Elimu
Video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Taarifa kwa Vyombo vya Habari
  • Mwongozo wa Matumizi ya TEHAMA Serikalini
  • Fomu ya Maombi ya Kusafiri Nje ya Nchi
  • MPANGO WA MANUNUZI MKOA WA SINGIDA
  • KUONA AJIRA ZA WAALIMU WA SAYANSI NA MAFUNDI SANIFU

Tovuti Muhimu

  • UTUMISHI
  • TAMISEMI
  • IKULU
  • WIZARA YA ELIMU
  • NECTA
  • WIZARA YA AFYA

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Ramani ya Mkoa

Wasiliana Nasi

    SINGIDA

    Anuani: P O BOX 5 SINGIDA

    Simu: 2502170, 2502089

    Simu: 2502170, 2502089

    Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Usiri
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani
    • Huduma

Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.