KATIBU Tawala Mkoa wa Singida, Dk. Fatuma Mganga, amewataka vijana kutokubali kutumika kwa kujiingiza katika mambo yasiyofaa na badala yake wajishughulishe katika shughuli za kiuchumi za uzalishaji mali kama kilimo ili kuinua vipato vyao na hivyo kufuta umasikini.
Akizungumza leo (Agosti 12, 2023) na vijana wa Mkoa wa Singida kwenye Maadhimisho ya Siku ya Vijana Duniani, alisema Serikali imeanzisha mradi wa ‘Building a Better Tomorrow’ (BBT) unaolenga kuongeza ushiriki wa vijana katika kilimo kwa kuwapatia mafunzo maeneo ya mashamba hivyo ni wakati sasa kwa vijana kuchangamkia fursa hiyo.
Dk. Mganga alisema mambo ya kushinda kwenye mitandao ya kijamii na kuilaumu Serikali kwamba haitupi fursa na kujenga fikra potofu kwamba kilimo ni kazi inayofanywa na watu ambao hawajasoma na masikini hayana msingi na hayawezi kusaidia kuinua uchumi wao.
“Vijana wa Singida msiwe vijana wa kulaumu kwamba Serikali haitupi fursa, hivi unataka Serikali ikusaidie hata kufuga kuku, vijana msitumike katika kazi zisizo na tija huko ni kukosa uzalendo, mkikubali kurubuniwa nchi itakosa wazalendo,” alisema.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.