Katika kuonyesha kuwa wanawake wanaweza,Mkuu wa Mkoa wa Singida, Halima Dendego, leo (Machi 4, 2025) amewaongoza wanawake wa Wilaya ya Singida kushiriki ujenzi wa shule ya amali ya Mkoa wa Singida inayojengwa kata ya Unyambwa Manispaa ya Singida kwa gharama ya Sh.bilioni 1.6 ikiwa ni mwendelezo wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani.
Akizungumza na wanawake waliojitokeza kushiriki ujenzi huo amesema kwamba Halmashauri zote za Mkoa huo zimepewa fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Amali ambayo watachaguliwa kujiunga wanafunzi wenye vipaji.
. "Tunamshukru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan,tumeona dhamira yake ya kweli kwa Watanzania ya kuweza kuwakwamua kiuchumi,shule hii ya Amali inayojengwa kata ya Unyambwa tutawachagua wenye vipaji ndio wajiunge ili watuletee mageuzi ya kiuchumi,alisema Mhe.Dendego
Mhe.Dendego amesema nchi yetu imezindua sera mpya ya elimu inayokwenda kuangalia vitendo na elimu ya nadharia lengo ili mwanafunzi anapohitimu masomo aweze kujiajiri au kuajiriwa akiwa tayari ana ujuzi mkubwa.
Aidha,Mkuu wa Mkoa wa Singida amezipongeza wilaya zote wa mkoa huu kwa kutekeleza maelekezo ya serikali katika kuadhimisha siku ya wanawake dunia kuanzia ngazi ya Kata hadi Mkoa ambayo yamewashirikisha wanawake kwa kufanya shughuli mbalimbali za maendeleo.
Awali Mhandisi wa Manispaa ya Singida amesema serikali imetoa Sh.Bilioni.1.6 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya amali ya Mkoa wa Singida ambayo itakapokamilika katika awamu ya kwanza itachukua wanafunzi takribani 400 wenye vipaji watakaofundishwa ufundi wa aina mbalimbali.
Akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida,Ameongoza mamia ya wanawake wa Wilaya ya Singida kushiriki ujenzi wa shule hiyo ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kilele chake ni Machi 8, 2025.
Amesema katika awamu ya kwanza ujenzi ambao unatarajia kukamilika Mei 29, 2025 majengo 22 yatajengwa yakiwamo madarasa nane,maabara 2,mabweni 4,karakana ya ujenzi na ufundi uashi na karakana ya ufundi magari na kuchomelea.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.