Mkuu wa Mkoa wa Singida, Mhe. Halima Dendego, leo (Octoba 11, 2024) ameonyesha mfano bora wa uongozi kwa kujiandikisha kwenye orodha ya wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa utakaofanyika Novemba 27, 2024.
Zoezi hilo limefanyika katika kituo cha kujindikisha cha Shule ya Msingi Sababasaba, kata ya Utemini Singida Mjini.
RC. Dendego, ameelezea tofauti kati ya zoezi lililopita la uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura na hili la Daftari la Wakazi, akisisitiza umuhimu wa uandikishaji huu kwa ajili ya uchaguzi wa wenyeviti wa mitaa na wajumbe wa kamati za mitaa, pamoja na viongozi wa vijiji na vitongoji.
“Hili ni zoezi tofauti na lile lililopita. Ikiwa hujajiandikisha hutoweza kumpigia kura kiongozi unayemtaka katika mtaa wako". Amesema RC Dendego.
Katika mwendelezo wa zoezi hilo, Mkuu wa mkoa huyo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi ili kujiorodhesha katika Daftari la Wakazi, ili waweze kuwachagua viongozi wanaowafaa katika maeneo yao huku akihimiza kila mmoja kuzingatia wajibu wake wa kisiasa akisisitiza kwamba sauti ya wananchi ni muhimu katika mchakato wa uchaguzi.
Zoezi hili lina umuhimu mkubwa katika kuhakikisha kuwa viongozi wanaoingia madarakani wanachaguliwa kwa njia ya haki na uwazi na kwamba kila raia anapata fursa ya kushiriki katika mchakato wa kisiasa.
SINGIDA
Anuani: P O BOX 5 SINGIDA
Simu: 2502170, 2502089
Simu: 2502170, 2502089
Barua Pepe: info@singida.go.tz ras@singida.go.tz
Copyright ©2023 Singida Regional Commisioner' Office . All rights reserved.